bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Romans 16
Romans 16
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
1
NAWAPENI sifa njema za Foibe ndugu yetu, aliye mwenye khuduma katika kanisa lilioko Kenkrea,
2
illi mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu, kwa sababu yeye nae amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia na mimi pia.
3
Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
4
waliokuwa tayari hatta kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, illa na makanisa ya mataifa yote pia;
5
nisalimieni kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.
6
Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yetu.
7
Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.
8
Nisalimieni Amplia, mpenzi wangu katika Bwana.
9
Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Staku, mpenzi wangu.
10
Nisalimieni Apelle, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumba ya Aristobulo.
11
Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumba ya Nakisso, walio katika Kristo.
12
Nisalimieni Trufina na Trufosa, wenye ijtihadi katika Kristo.
13
Nisalimieni Rufo, mteule katika Kristo, na mama yake, aliye mama yangu pia.
14
Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao.
15
Nisalimieni Filologo na Julia, Nereu na ndugu yake, na Olumpa, na watakatifu wote walio pamoja nao.
16
Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.
17
Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
18
Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.
19
Maana utii wenu umewafikilia watu wote; bassi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka mwe wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
20
Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
21
Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu.
22
Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana.
23
Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.
24
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amin.
25
Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,
26
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;
27
yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16