bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Romans 15
Romans 15
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
1
BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu.
2
Killa mtu miongoni mwetu ampendeze jirani yake apate wema akajengwe.
3
Kwa maana Kristo nae hakujipendeza nafsi yake; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu yalinipata mimi.
4
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.
5
Na Mungu mwenye uvumilivu na faraja awajalieni kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa namna ya Yesu Kristo;
6
illi kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa liwima wetu Yesu Kristo.
7
Kwa hiyo mkaribishane, kama nae Kristo alivyotukaribisha, illi Mungu atukuzwe.
8
Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu;
9
nao Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa sababu hii nitakusifu katika Mataifa, Na jina lako nitaliimba.
10
Na tena anena, Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.
11
Na tena, Msifuni Bwana, Mataifa wote; Mpeni sifa watu wote.
12
Na tena Isaya anena, Litakuwa shina la Yesse, Nae aondokeae kuwatawala Mataifa; ndiye Mataifa watakaemtumaini.
13
Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.
14
Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.
15
Lakini nimewaandikieni, ndugu zangu, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu kana kwamba nawakumbusheni, kwa neema ile niliyopewa na Mungu,
16
illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
17
Bassi, nina sababu ya kujisifu katika Kristo Yesu mbele za Mungu.
18
Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,
19
katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,
20
kadhalika nikijitahidi kuikhubiri Injili, nisikhubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine,
21
bali kama ilivyoandikwa, Wale wasiokhubiriwa khahari zake wafaona, Na wale wasiosikia watafahamu.
22
Ndio sababu nalizuiwa marra nyingi nisije kwenu.
23
Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mengi nikiwa na shauku kuja kwenu;
24
wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo.
25
Na sasa ninakwenda Yerusalemi, nikiwakhudumu watakatifu;
26
maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu katika Yerusalemi walio maskini.
27
Naam, imewapendeza, tena wanawiwa nao. Kwa maana ikiwa mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwakhudumu kwa mambo yao ya mwili.
28
Bassi nikiisha kumaliza hazi hii, na kuwatilia muhuri tunda hili, nitapita kwenu na kutoka kwenu nitakwenda Hispania.
29
Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa haraka ya Injili ya Kristo.
30
Nakusihini, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami kwa maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu,
31
niokolewe nao waasio katika Yahudi, na tena khuduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemi ipate kibali kwa watakatifu,
32
nipate kufika kwenu kwa furaha, kama Mungu akipenda, nikapate kupumzika pamoja nanyi.
33
Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amin.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16