bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
2 Chronicles 1
2 Chronicles 1
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 2 →
1
Solomoni mwana wa Daudi alijiimarisha kwenye milango yote! Katika ufalme wake, kwa kuwa BWANA Mungu wake alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu mno.
2
Ndipo Solomoni akasema na Israeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa.
3
Naye Solomoni na kusanyiko lote wakakwea mpaka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kwa kuwa huko ndiko hema la Mungu la Mkutano lilipokuwa, ambalo Mose mtumishi wa BWANA alikuwa amelitengeneza huko jangwani.
4
Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu mpaka mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu.
5
Lakini ile madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza ilikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya BWANA Mungu, hivyo Solomoni na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko.
6
Solomoni akapanda huko ilikokuwa madhabahu ya shaba mbele za BWANA katika Hema la Kukutania na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake.
7
Usiku ule Mungu akamtokea Solomoni na kumwambia, “Omba lo lote unalotaka nami nitakupa.”
8
Solomoni akamjibu Mungu, “Umemwonyesha baba yangu Daudi fadhili nyingi nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake.
9
Sasa, BWANA Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi.
10
Nakuomba unipe mimi hekima na maarifa, ili niweze kuongoza watu hawa, kwa kuwa ni nani awezaye kutawala hawa watu wako walio wengi hivi?”
11
Mungu akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao,
12
kwa hiyo utapewa hekima na maarifa. Tena nitakupa pia mali, utajiri na heshima ambayo hakuna mfalme ye yote aliyekuwepo kabla yako amewahi kuwa navyo na hakuna ye yote baada yako atakayekuwa navyo.”
13
Ndipo Solomoni akaenda mpaka Yerusalemu kutoka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kutoka mbele ya Hema la Kukutania. Naye akatawala juu ya Israeli.
14
Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari ya vita 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari ya vita na mengine akawanayo huko Yerusalemu.
15
Mfalme akaongeza fedha na dhahabu vikawa vitu vya kawaida kama vile mawe huko Yerusalemu, nayo mierezi ikawa mingi kama miti ya mikuyu chini ya vilima.
16
Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue. Wafanya biashara wa kifalme waliwanunua kutoka Kue.
17
Walileta magari ya vita kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha kwa kila moja, na kwa kila farasi shekeli 150. Pia wakawapeleka ili kuwauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36