bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
2 Chronicles 5
2 Chronicles 5
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
1
Hivyo kazi yote Solomoni aliyofanya kwa ajili ya Hekalu la BWANA ikamalizika, Solomoni akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu, yaani, fedha, dhahabu na vyombo vingine vyote na kuviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.
2
Kisha Mfalme Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili kulipandisha Sanduku la Agano la BWANA kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.
3
Nao watu wote wa Israeli wakaja pamoja kwa mfalme wakati wa sikukuu katika mwezi wa saba.
4
Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamefika, Walawi wakaliinua Sanduku la Agano,
5
nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, ambao walikuwa ni Walawi walivibeba vitu hivyo,
6
naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli lililokuwa limemkusanyikia walikuwa mbele ya Sanduku, wakitoa dhabihu nyingi za kondoo na ng'ombe ambazo hazikuwezekana kuandikwa wala kuhesabiwa.
7
Kisha makuhani wakaleta Sanduku la Agano la BWANA mpaka mahali pake ndani ya mahali Patakatifu pa Hekalu, yaani, mahali Patakatifu pa Patakatifu na kuliweka chini ya mabawa ya wale makerubi.
8
Makerubi walitanda mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea.
9
Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zingeweza kuonekana ukiwa ndani mbele ya mahali Patakatifu, lakini siyo ukiwa nje ya mahali patakatifu, nayo hiyo mipiko ipo mpaka leo.
10
Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine cho chote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali BWANA alipofanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
11
Basi makuhani wakaondoka hapo mahali patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao.
12
Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta.
13
Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru BWANA, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu BWANA wakisema: “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo Hekalu la BWANA likajazwa na wingu,
14
nao makuhani hawakuweza kusimama kufanya huduma yao kwa sababu ya wingu, kwa maana utukufu wa BWANA ulilijaza Hekalu la Mungu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36