bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
2 Chronicles 22
2 Chronicles 22
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 23 →
1
Watu wa Yerusalemu wakamfanya Ahazia, mdogo wa wote wa wana wa Yerohamu, kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwa sababu washambuliaji wa ghafula waliokuwa wameingia kambini pamoja na Waarabu, walikuwa wamewaua wana wakubwa wote wa Yehoramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
2
Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia mjukuu wa kike wa Omri.
3
Ahazia naye akaziendea njia za nyumba ya Ahabu kwa sababu mama yake alikuwa mshauri wake katika kutenda maovu.
4
Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA kama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake nyumba ya Ahabu ndio waliokuwa washauri wake, kwa uangamivu wake.
5
Pia akafuata shauri lao alipokwenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu,
6
hivyo akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyokuwa ameyapata huko Ramoth, kwenye vita vyake na Hazaeli mfalme wa Aramu. Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.
7
Mungu alikuwa ameamuru kwamba kuanguka kwa Ahazia kungetokea atakapokwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alikuwa amemtia mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu.
8
Yehu alipokuwa anatekeleza hukumu juu ya nyumba ya Ahabu, akawakuta wakuu wa Yuda na wana wa jamaa ya Ahazia waliokuwa wanamhudumia Ahazia, naye akawaua.
9
Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamwua. Wakamzika kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta BWANA kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme.
10
Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akaondoka akawaua wazao wote wa kifalme wa nyumba ya Yuda.
11
Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia na kumwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa wanakaribia kuuawa. Akamweka yeye pamoja na yaya wake kwenye chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, mkewe Kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha mtoto ili Athalia asimwue.
12
Akawa pamoja nao akiwa amefichwa katika Hekalu la Mungu kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alipokuwa anatawala nchi.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36