bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
2 Chronicles 15
2 Chronicles 15
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 16 →
1
Roho wa BWANA akamjia Azaria mwana wa Obedi.
2
Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. BWANA yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi.
3
Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria.
4
Lakini katika taabu yao walimrudia BWANA, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao.
5
Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa ye yote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa.
6
Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.
7
Lakini kwa habari yenu ninyi, iweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.”
8
Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Obedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka katika miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya BWANA iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la BWANA.
9
Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba BWANA Mungu wake alikuwa pamoja naye.
10
Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Asa.
11
Wakati huo wakamtolea BWANA dhabihu za ng'ombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka katika zile nyara walizoteka.
12
Wakafanya agano kumtafuta BWANA, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote.
13
Wale wote ambao hawangemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke.
14
Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu.
15
Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo BWANA akawastarehesha pande zote.
16
Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake asiwe mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza kichakani nguzo ya chukizo ya Ashera. Asa akaikata ile nguzo akaiangusha, akaivunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.
17
Ingawa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, Asa akauweka moyo wake wote kwa BWANA kikamilifu siku zote za maisha yake.
18
Akaleta katika Hekalu la Mungu fedha, dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.
19
Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36