bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 John 1
1 John 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
*Yaliyokuwapo tangu mwanzo, tuliyoyasikia, tuliyoyaona kwa macho yetu, tuliyoyatazama na kuyapapasa kwa mikono yetu, ndiyo, tunayoyatangaza kuwa Neno lenye uzima.
2
Nao uzima ulifunuliwa, nasi tukauona, kwa hiyo twashuhudia kwa kuwatangazia ninyi huo uzima wa kale na kale uliokuwa kwa Baba, ukatufunuliwa sisi.
3
Basi, tuliyoyaona, tuliyoyasikia, twawatangazia hata ninyi, nanyi mpate kuwa mwenzetu wa bia. Nayo bia yetu sisi ni ile ya Baba na ya Mwana wake Yesu Kristo.
4
Haya tunawaandikia ninyi, furaha yenu itimizwe.*
5
Nao utume, tuliousikia kwake, tunaowatangazia ninyi, ndio huu: Mungu ni mwanga, namo mwake hamna giza iwayo yote.
6
Tukisema: Tuko na bia naye, kisha tunaendelea gizani, twasema uwongo, nayo yaliyo ya kweli hatuyafanyi.
7
Lakini tukiendelea mwangani, kama yeye alivyo mwangani, tuko na bia yetu sisi kwa sisi, nayo damu ya Yesu, Mwana wake, hututakasa, makosa yote yatutoke.
8
Tukisema: Makosa hatunayo, tunajidanganya wenyewe, nayo kweli haimo mwetu.
9
Lakini tukiyaungama makosa yetu, yeye ni mwelekevu na mwongofu, atuondolee makosa, kisha atutakase, upotovu wote ututoke.
10
Tukisema: Hatukukosa, twamfanya yeye kuwa mwongo, tena Neno lake halimo mwetu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5