bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 John 4
1 John 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
Wapendwa, msiitikie kila roho, ila zijaribuni roho, kama zimetoka kwa Mungu! Kwani wafumbuaji wa uwongo wengi wametokea ulimwenguni.
2
Hapo ndipo, mtakapoitambua roho ya Mungu: kila roho inayoungama, ya kuwa Yesu Kristo amekuja mwenye mwili wa kimtu, imetoka kwa Mungu.
3
Lakini kila roho isiyomwungama Yesu haikutoka kwa Mungu. Hiyo ndiyo roho ya Mpinga Kristo, mliyoisikia, ya kuwa inakuja; tena sasa imekwisha kuwamo humu ulimwenguni.
4
Vitoto, ninyi m wa Kimungu, tena mmewashinda wale, kwani yeye alimo mwenu ni mkubwa kuliko yeye aliomo humu ulimwenguni.
5
Wale ni wa kiulimwengu; kwa hiyo husema ya kiulimwengu, nao wa kiulimwengu huwasikia.
6
Sisi tu wa Kimungu; naye amtambuaye Mungu hutusikia sisi, lakini asiye wa Kimungu hatusikii sisi. Hapo twaitambua roho, kama ni ya kweli au ya upotevu.
7
Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi! Kwani upendo ni wa Kimungu. Kila mwenye kupenda amezaliwa naye Mungu, naye humtambua Mungu.
8
Asiyependa hakumtambua Mungu kwamba: Mungu ni upendo.
9
*Upendo wake Mungu wa kutupenda sisi umeonekana waziwazi hapo, Mungu alipomtuma Mwana wake wa pekee kuja ulimwenguni, sisi tupewe naye uzima.
10
Humu ndimo upendo: sio sisi tuliompenda Mungu, ila yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwana wake kuwa kole kwa ajili ya makosa yetu.
11
Wapendwa, kama Mungu alitupenda hivyo, imetupasa nasi kupendana.
12
Hakuna mtu aliyemwona Mungu hata kale; tukipendana, Mungu hukaa mwetu, upendo wake ukatimilika mwetu.
13
Hapa ndipo, tunapotambua, kama tumo mwake yeye, kama yeye naye yumo mwetu, tukiwa na Roho wake, ambaye alitugawia.
14
Nasi tumeviona, tukavishuhudia, ya kuwa Baba amemtuma Mwana, awe mwokozi wa ulimwengu.*
15
Ye yote atakayeungama kwamba: Yesu ni mwana wake Mungu, basi, Mungu hukaa mwake huyo, naye mwake Mungu.
16
Nasi tumeutambua, tukautegemea upendo wake Mungu wa kutupenda sisi. *Mungu ni upendo; naye mwenye upendo hukaa mwake Mungu, naye Mungu hukaa mwake yeye.
17
Upendo, tupendwao nao, unatimilika hapo, tukiweza kuishangilia siku ya hukumu; kwani yeye alivyo, ndivyo, tulivyo na sisi humu ulimwenguni.
18
Woga haumo katika upendo, ila upendo uliotimilika huufukuza woga, kwa sababu woga huhangaisha. Naye aliye mwenye woga bado hajautimiliza upendo.
19
Sisi na tumpende! Kwani yeye alianza kutupenda sisi.
20
Mtu akisema: Nampenda Mungu, akamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwani asipompenda ndugu yake, anayemwona, hawezi kumpenda Mungu, asiyemwona,
21
maana agizo hili tumepewa naye kwamba: Mwenye kumpenda Mungu sharti ampende na ndugu yake!*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5