bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 John 2
1 John 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
1
Ninyi vitoto, mlio wangu, haya nawaandikiani, msikose. Lakini kama yuko aliyekosa, tunaye mwombezi kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwongofu.
2
Naye ndiyo kole iliyotolewa kwa ajili ya makosa yetu, lakini si kwa ajili ya makosa yetu tu, ila hata kwa ajili ya makosa ya ulimwengu wote.
3
Namo humu ndimo, tutambuamo, ya kuwa tumemtambua, tukiyashika maagizo yake.
4
Mtu akisema: Nimemtambua, lakini maagizo yake hayashiki, mtu huyo ni mwongo, nayo kweli haimo mwake.
5
Lakini mtu akilishika Neno lake, mwake yeye upendo wa Mungu umetimia kweli. Humu ndimo, tutambuamo, kama tumo mwake.
6
Mtu anayesema: Nafuliza kuwa mwake, huyo inampasa kufanya mwenendo, kama yeye alivyofanya mwenendo.
7
Wapendwa, siwaandikii agizo jipya, ila agizo la kale, mlilokuwa nalo tangu mwanzo. Agizo hilo la kale ndilo Neno, mlilosikia.
8
Tena nawaandikia agizo jipya lililo kweli mwake namo mwenu ninyi, kwamba: Giza hupita, nao mwanga wa kweli umekwisha kumulika.
9
Mtu akisema: Nimo mwangani, akamchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa hivi.
10
Mwenye kumpenda ndugu yake hukaa mwangani, asiwe na kwazo lililomo mwake.
11
Lakini mwenye kumchukia ndugu yake yumo gizani na kuendelea gizani, asijue, anakokwenda, kwani giza imempofusha macho yake.
12
Nawaandikia ninyi mlio vitoto, kwani mmeondolewa makosa yenu kwa ajili ya jina lake.
13
Nawaandikia ninyi mlio baba, kwani mmemtambua yeye aliye mwenye kuwapo tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi mlio vijana, kwani mmemshinda yule Mbaya.
14
Naliwaandikia ninyi mlio wana, kwani mmemtambua Baba. Naliwaandikia ninyi mlio baba, kwani mmemtambua yeye aliye mwenye kuwapo tangu mwanzo. Naliwaandikia ninyi mlio vijana, kwani mko na nguvu, hata Neno la Mungu linakaa mwenu, nanyi mmemshinda yule Mbaya.
15
Msiupende ulimwengu huu, wala vilivyomo ulimwenguni! Mtu akiupenda ulimwengu huu, upendo wa Baba haumo mwake huyo.
16
Kwani vyote vilivyomo ulimwenguni: tamaa za miili nazo tamaa za macho nayo mambo makuu, watu wanayojivunia, havikutoka kwake Baba, ila ulimwenguni.
17
Ulimwengu huu utapita pamoja na tamaa zake; lakini ayafanyaye, Mungu ayatakayo, hukaa kale na kale.*
18
Vitoto, sasa ni saa ya mwisho. Kama mlivyosikia, ya kuwa Mpinga Kristo anakuja, sasa wapinga Kristo wamekwisha kuwapo wengi; kwa hiyo twatambua, ya kuwa ni saa ya mwisho.
19
Walitoka kwetu sisi, lakini hawakuwa wa kwetu; kwani kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka, kusudi waonekane waziwazi, ya kuwa hao wote sio wa kwetu.
20
Nanyi mmemiminiwa mafuta naye aliye Mtakatifu, mkayajua yote.
21
Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamkuyajua yaliyo ya kweli, ila kwa sababu mmeyajua, tena mmejua, ya kuwa hakuna uwongo utokao kwenye ukweli.
22
Tena yuko nani aliye mwongo, asipokuwa yeye anayekana kwamba: Yesu siye Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo anayemkana Baba na Mwana.
23
Kila anayemkana Mwana hata Baba hanaye vilevile; lakini anayemwungama Mwana anaye hata Baba.
24
Nanyi mliyoyasikia tangu mwanzo, sharti yakae mwenu! Hayo, mliyoyasikia tangu mwanzo, yakikaa mwenu, hata ninyi mtakaa mwake Mwana namo mwake Baba.
25
Nacho kiagio, alichotuagia mwenyewe, ndicho hiki: uzima wa kale na kale.
26
Haya nimewaandikia ninyi kwa ajili yao wanaowapoteza.
27
Yale mafuta, mliyomiminiwa naye, huwakalia, msifundishwe tena na mtu; ila kama mafuta yake yalivyowafundisha mambo yote, ndivyo, yalivyo kweli, huu si uwongo. Kwa hiyo yakalieni, kama yalivyowafundisha ninyi.
28
Sasa, vitoto, kaeni mwake yeye, tupate kushangilia, atakapotokea waziwazi, tusipatwe na soni naye hapo, atakaporudi!
29
Mkijua, ya kuwa yeye ni mwongofu, na mtambue, ya kuwa kila anayefanya wongofu amezaliwa naye yeye!
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5