bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 John 5
1 John 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
1
*Kila mwenye kuyategemea ya kwamba: Yesu ni Kristo, amezaliwa na Mungu. Naye kila mwenye kumpenda mzazi aliyemzaa humpenda hata yeye aliyezaliwa naye.
2
Hapo ndipo, tunapotambua, kama tunawapenda wana wa Mungu, tukimpenda Mungu na kufanya maagizo yake.
3
Kwani kumpenda Mungu ni kuyashika maagizo yake, nayo maagizo yake si magumu.
4
Kwani kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Nako kunakotushindisha ulimwengu ndiko kumtegemea Mungu.
5
Yuko nani anayeushinda ulimwengu, asipokuwa mwenye kuyategemea ya kwamba: Yesu ni Mwana wake Mungu?*
6
Huyu Yesu Kristo ndiye aliyekuja mwenye maji na damu; hakuja na maji tu, ila alikuja mwenye maji na damu. Naye Roho ndiye anayeyashuhudia, kwani Roho ndiye kweli.
7
Kwa hiyo wako watatu wanaoshuhudia mbinguni: Baba na Neno na Roho Mtakatifu; nao hawa watatu ni mmoja. Tena wako watatu wanaoshuhudia nchini: Roho na Maji na Damu;
8
hao watatu nao wamepatana ushahidi kuwa mmoja.
9
*Tukiuitikia ushuhuda wa watu, basi, ushuhuda wa Mungu ni mkubwa zaidi, kwani ushuhuda wa Mungu ndio huo, aliomshuhudia Mwana wake mwenyewe.
10
Mwenye kumtegemea Mwana wa Mungu huo ushuhuda anao mwake. Asiyemtegemea Mungu amemfanya kuwa mwongo yeye, kwani hakuutegemea ushuhuda, Mungu aliomshuhudia Mwana wake mwenyewe.
11
Nao ushuhuda ndio huu wa kwamba: Mungu ametupa uzima wa kale na kale; uzima huu umo mwake Mwana wake yeye.
12
Aliye naye Mwana, anao hata uzima; asiye naye Mwana wa Mungu, hata uzima hanao.
13
Haya nimewaandikia ninyi mnaolitegemea Jina la Mwana wa Mungu, mpate kujua: uzima wa kale na kale mnao.
14
Kunakotupa moyo wa kumjia wenye furaha ndiko kujua, yo yote, tutakayomwomba kwa hayo, ayatakayo, hutusikia.
15
Nasi tukijua, ya kuwa anatusikia yo yote, tutakayomwomba, twajua: maombo, tuliyomwomba, tumekwisha kupewa.*
16
Mtu akimwona ndugu yake, akikosa kosa lisiloua, na amwombee; ndipo, Mungu atakapompa uzima pamoja na wakosaji wenziwe wafanyayo yasiyoua. Liko kosa linaloua; hapo sisemi, mtu amwombee.
17
Upotovu wote ni wa kukosa, tena yako makosa yasiyoua.
18
Twajua: kila aliyezaliwa na Mungu hakosi, ila aliyezaliwa na Mungu hujiangalia, yule Mbaya asimguse.
19
Twajua: sisi tu wa Kimungu, lakini ulimwengu wote umo katika nguvu ya yule Mbaya.
20
Nasi twajua: Mwana wa Mungu amekuja, akatupa mawazo ya kumtambua mwenye kweli. Nasi tumo mwake mwenye kweli, ndimo mwake Yesu Kristo, Mwana wake. Huyu ndiye Mungu wa kweli na uzima wa kale na kale.
21
Vitoto, jiangalieni, msije kutambikia vinyago! Amin.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
All chapters:
1
2
3
4
5