bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Peter 2
1 Peter 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
1
*Jivueni uovu wote na udanganyi wote na ujanja na kijicho na mateto yote!
2
Kwa kuwa m vitoto vichanga vilivyozaliwa siku hizi, yatakeni maziwa ya kweli yasiyodanganya, mkuzwe nayo, mpaka mwufikie wokovu,
3
mkiwa mmeonja, mkaona, ya kuwa Bwana ni mwema!
4
Huyu mjieni! Maana ni jiwe lenye uzima. Kweli watu walilikataa, lakini Mungu amelichagua kuwa lenye heshima.
5
Nanyi mlio kama mawe yenye uzima mjengwe kuwa nyumba ya Kiroho, mwe watambikaji watakatifu wa kumtolea Mungu vipaji vya tambiko vya kiroho vimpendezavyo kwa ajili ya Yesu Kristo!
6
Kwa hiyo imeandikwa katika Maandiko kwamba: Tazameni, naweka humu Sioni jiwe la pembeni lililochaguliwa kuwa lenye heshima, naye alitegemeaye hatatwezeka.
7
Kwa hiyo ninyi mlitegemealo hupata heshima, lakini wasiolitegemea jiwe hili, waashi walilolikataa, hilihili huwa kwao jiwe la pembeni kwamba:
8
Ni jiwe la kujigongea na mwamba wa kujikwalia. Nao hujigonga, kwa sababu hawalitii Neno; navyo ndivyo, walivyowekewa.
9
Lakini ninyi m ukoo uliochaguliwa, m watambikaji wa kifalme, m chama kitakatifu, m watu wakombolewao, mpate kuyatangaza mema yake yeye aliyewaita, mtoke gizani, mwingie mwangani mwake mlimo na mastaajabu.
10
Kale hamkuwa ukoo mmoja, lakini sasa mmekuwa ukoo wake Mungu. Tena kale mlikuwa hamjui kuhurumiwa, lakini sasa mmekwisha kuhurumiwa.*
11
*Wapendwa, kwa sababu m wageni wanaopita tu, nawaonya ninyi, mziepuke tamaa za miili zinazozigombanisha roho zenu!
12
Fanyeni mwenendo ulio mzuri kwa wamizimu! Hivyo wale wanaowasingizia ninyi kuwa watenda maovu, wanapoziona kazi zenu nzuri, watamtukuza Mungu siku ile, atakapowatokea kuwakagua.
13
Kwa ajili ya Bwana utiini ukuu wote uliowekwa na watu: Akiwa mfalme, maana huwapita wote!
14
Wakiwa viongozi, maana hutumwa naye kulipiza watenda maovu na kuwapa sifa watenda mema!
15
Nayo ndiyo, Mungu ayatakayo, matendo yenu mema yaunyamazishe upuzi wa watu wajinga.
16
Kwani mmekwisha kukombolewa, lakini huko kukombolewa, msikugeuze kuwa kifuniko cha kuuficha uovu, ila mjulike kuwa watumwa wake Mungu!
17
Wote waheshimuni! Wapendeni ndugu! Mwogopeni Mungu! Mheshimuni mfalme!
18
Ninyi watumishi, watiini mabwana zenu na woga wote! Msiwatii wale tu walio wema na wapole, ila nao walio wakali!
19
Kwani huko ni kugawiwa chema, mtu ateswaye kwa kupotolewa akiyavumilia hayo masikitiko kwa kuwa wake Mungu.
20
Kwani ni chema gani cha kukivumisha, mkiyavumilia mapigo, myapatayo kwa sababu ya kukosa? Lakini mkiyavumilia mateso yawapatayo kwa sababu ya kutenda mema, hiki ndicho chema, Mungu alichowagawia.*
21
*Maana ndiyo mliyoitiwa. Kwani Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachilia kielezo, mpate kufuata nyayo zake.
22
Yeye hakufanya lenye kukosa, uwongo tu haukuonekana kinywani mwake.
23
Alipotukanwa hakutukana naye, alipoteseka hakutisha, ila aliyapeleka kwake yeye anayehukumu kwa kweli.
24
Aliyachukua mwenyewe makosa yetu, nao mwili wake ndio ulioyakweza mtini, sisi tupate kuyaepuka makosa na kuukalia wongofu, namo katika mavilio yake ndimo, mlimoponea.
25
Kwani mlikuwa kama kondoo waliopotea. Lakini sasa mmegeuzwa, mmwelekee mchungaji na mkaguzi wa roho zenu.*
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5