bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Peter 4
1 Peter 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
Kwa sababu Kristo aliteswa mwilini kwa ajili yetu, jipeni nanyi mioyo iliyo hivyo, iwashindishe! Kwani atesekaye mwilini huacha kukosa,
2
nazo siku zake zilizosalia za kuwapo mwilini hatazimaliza na kuzifuata tamaa za watu, ila atafanya, Mungu ayatakayo.
3
Kwani inatosha, ya kuwa siku zilizopita mmeyafanya, wamizimu wayatakayo, mkifuata uasherati na tamaa na ulevi na ulafi na unywaji na matambiko ya vinyago yamchukizayo Mungu.
4
Wale wanayastukia, ya kuwa sasa hamfuatani nao na kujipujua pasipo kiasi; kwa hiyo wanawatukana.
5
Lakini atakayewalipiza ni yeye aliye tayari kuwahukumu wanaoishi nao waliokufa.
6
Kwani kwa hiyo hata wafu walipigiwa mbiu njema, wahukumiwe kimwili, kama iwapasavyo watu, kisha wapate kuwapo kiroho, kama Mungu anavyokuwapo.
7
Mwisho wa vitu vyote uko karibu. Kwa hiyo mjiangalie, mlevuke, mpate kuomba!
8
*Lakini kupita yote: jikazeni kupendana wenyewe! Kwani upendano hufunika makosa mengi.
9
Mkaribishane pasipo kunung'unika!
10
Mtumikiane ninyi kwa ninyi, kila mtu akikitumia chema chake, alichogawiwa! Hivyo mtakuwa watunzaji wazuri wa yale mema mengi ya Mungu.
11
Mtu akisema na ayaseme, kama ni kusema maneno ya Mungu! Mtu akitumika na atumike kwa kuwa mtu aliyepewa nguvu na Mungu kwamba: Katika mambo yote Mungu atukuzwe kwa ajili ya Yesu Kristo! Wake yeye ni utukufu na uwezo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*
12
*Wapendwa, msistuke kama wenye kuona neno geni mkipatwa na mambo yenye moto! Maana mtajaribiwa tu.
13
Ila mkiwa wenzake Kristo wa kuteseka changamkeni! Maana hapo, utukufu wake utakapotokea waziwazi, ndipo, mtakapochangamka na kushangilia.
14
M wenye shangwe mkitukanwa kwa kuwa mnalo Jina lake Kristo. Kwani Roho wa utukufu na na wa Mungu anawakalia.
15
Lakini kwenu asioneke ateswaye kwa kuwa mwuaji au mwizi au mtenda maovu au mkaguzi wa mambo yasiyo yake!
16
Lakini mtu akiteseka kwa kuwa Mkristo, asione soni, ila amtukuze Mungu kwa kuwamo katika Jina hili!
17
Kwani siku zimetimia, hukumu ianze kwao walio wa Nyumba ya Mungu. Basi, ikianza kwetu itakuwaje mwishoni kwao waliokataa kutii Utume mwema wa Mungu?
18
Tena mwongofu akiona: kuokoka ni kugumu, asiyemcha Mungu na mkosaji atapona wapi?
19
Kwa hiyo nasema: Wenye kuteseka kwa hayo, Mungu aliyoyataka, watende mema! Hivyo wataweza kumwagizia yeye roho zao, maana ni muumbaji mwelekevu.*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5