bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Peter 5
1 Peter 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
1
Wazee walioko kwenu nawaonya mimi niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso yake Kristo, nitakayekuwa mwenziwe hata katika utukufu utakaofunuliwa.
2
Nawaonya kwamba: Lichungeni kundi la Mungu lililoko kwenu, si kwa shuruti, ila kwa kuyapenda wenyewe, Mungu ayatakayo, wala si kwa kufuata machumo mabaya, ila kwa mioyo!
3
Msiwatawale wateule, ila mwe vielezo vya kikundi cha kwenu!
4
Mkiwa hivyo mtapewa kilemba chenye utukufu kisichonyauka, hapo, mchungaji mkuu atakapotokea waziwazi.
5
Vilevile ninyi mlio watu wazima, watiini wazee!* Nyote tumikianeni kila mtu na mwenziwe, kama ni mtumwa wake kwa kujinyenyekeza! Kwani wenye kujikweza Mungu huwapingia, lakini wanyenyekevu huwapatia huruma.
6
Kwa hiyo unyenyekeeni mkono wa Mungu ulio wenye nguvu, yeye awakweze, siku yake itakapofika!
7
Mtupieni Mungu yote, myahangaikiayo! Kwani yeye huwatunza.
8
Levukeni, mkeshe! Kwani mpingani wenu Satani huzunguka kama simba anayenguruma akitafuta, atakayemmeza.
9
Huyo mgombanisheni kwa nguvu ya kumtegemea Mungu mkijua, ya kuwa mateso yayo hayo huwapata nao ndugu zenu walioko ulimwenguni!
10
Naye Mungu mwenye mema yote ya kuwagawia, aliyewaitia nanyi utukufu wake wa kale na kale uliomo katika Kristo, atawalinganya mwenyewe, mkiteseka kidogo, na kuwapa uwezo na nguvu na msingi mgumu.
11
Wake yeye ni utukufu na uwezo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*
12
Nimewaandikia kidogo kwa mkono wa ndugu Silwano, ninayemwona kuwa mwelekevu. Nimewaonya na kuwashuhudia kwamba: Mmegawiwa mema ya Mungu yaliyo ya kweli. Nayo yakalieni!
13
Wateule waliomo humu Babiloni pamoja nasi wanawasalimu, hata mwanangu Marko.
14
Mwamkiane na kunoneana kwa kupendana! Utengemano uwakalie nyote mlio wake Kristo!
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
All chapters:
1
2
3
4
5