bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Peter 3
1 Peter 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
1
Vivyo hivyo nanyi wake sharti mwatii waume wenu! Maana kama wako wasiolitii Neno, watatekwa kwa mwenendo wa wake zao pasipo kuambiwa maneno,
2
wakiona kwa macho yao, mnavyoendelea king'avu kwa kuwaogopa.
3
Nayo marembo yao yasiwe ya miili, kama misuko ya nywele na mapambo ya dhahabu na mavazi ya nguo nzuri!
4
Ila uzuri wao uwe wa mioyoni unaojificha mle ndani pasipo kuangamia, maana ni wa mtu mwenye roho ya upole na ya utulivu, naye Mungu huuona kuwa mali kweli.
5
Kwani hata kale wanawake watakatifu waliomngojea Mungu walijipamba hivyo wakiwatii waume wao,
6
kama Sara alivyomtii Aburahamu akimwita bwana. Nanyi wanawake, mnakuwa watoto wake mkitenda mema pasipo kuogopa vituko vyo vyote.
7
Vilevile nanyi waume, mwendeleane na wake zenu na kuwatambua kuwa viumbe vinyonge kuliko ninyi! Tena waheshimuni! Maana nao watagawiwa urithi wao wa uzimani pamoja nanyi; fanyeni hivyo, msizuiliwe kuomba!
8
*Kisha nyote mioyo yenu sharti iwe mmoja, mpate kuvumiliana na kupendana kama ndugu walio wenye uororo na unyenyekevu!
9
Msimlipe mtu uovu kwa uovu, wala matukano kwa matukano! Ila wafanyao hivyo mwaombee mema! Kwani hayo ndiyo, mliyoitiwa, mwirithi mbaraka.
10
Maana atakayependa kuwa uzimani naye atakaye kuona siku njema aulindie ulimi wake, usiseme mabaya, nayo midomo yake, isiseme madanganyifu!
11
Yaliyo mabaya ayaepuke, afanye mema, atafute penye utengemano, apakimbilie!
12
Maana macho ya Bwana huwatazama walio waongofu, masikio yake huyasikia maombo yao. Lakini uso wa Bwana huwapingia wafanyao mabaya.
13
Yuko nani atakayewaponza ninyi, mkijikaza kufanya mema?
14
Lakini ijapo mteswe kwa ajili ya wongofu mtakuwa wenye shangwe. Lakini msiyaogope maogopesho yao, wala msiyahangaikie!
15
Ila mtakaseni Bwana Kristo mioyoni mwenu!* Tena po pote mwe tayari kumjibu kila mtu anayewauliza kwa ajili ya kingojeo chenu kilichomo mwenu! Lakini wajibuni kwa upole na kuwaogopa!
16
Mioyo yenu sharti ijulike kuwa miema! Hivyo wenye kuwasengenya kwamba: M waovu, wataingiwa na soni kwa ajili ya mwenendo wenu, ukiwa mzuri kwa nguvu ya Kristo.
17
Kwani kuteswa kwa ajili ya kutenda mema, Mungu akivitaka, ni vizuri kuliko kuteswa kwa ajili ya kutenda maovu.
18
Kwani naye Kristo alikufa mara moja kwa ajili ya makosa yetu; yeye aliyekuwa mwongofu alikufa kwa ajili yetu tulio wapotovu, atupeleke kwake Mungu. Aliuawa kimwili, lakini alirudishwa uzimani Kiroho.
19
Hapo aliwaendea wazimu nao mle, waliomo kifungoni, akawapigia mbiu
20
wale waliokataa kutii kale, Mungu alipowangoja na kuwavumilia siku zile za Noa, kile chombo kikubwa kilipotengenezwa; lakini miongoni mwao wakaokoka wachache, watu wanane tu katika kondo ile ya maji.
21
Maji hayo ni mfano wa maji ya ubatizo yanayowaokoa sasa hata ninyi; kweli hayaondoi machafu ya miili, ila ya mioyo, ipate kuwa miema na kupatana naye Mungu kwa nguvu ya ufufuko wake Yesu Kristo.
22
Yeye yuko kuumeni kwa Mungu, maana amekwenda mbinguni, atiiwe nao malaika na wenye nguvu na wenye uwezo.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5