bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Thessalonians 1
1 Thessalonians 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
Sisi Paulo na Silwano na Timoteo tunawaandikia ninyi mlio wateule wa Tesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Upole uwakalie na utengemano!
2
Tunamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote. Nasi hatuachi kuwakumbuka katika kuomba kwetu
3
tukikumbuka mbele ya Mungu aliye Baba yetu, mnavyofanya kazi kwa kumtegemea, tena mnavyojisumbua, mpate kupendana, tena mnavyovumilia na kumngojea Bwana wetu Yesu Kristo.
4
Kwani ndugu mliopendwa na Mungu, twajua: mmechaguliwa.
5
Kwani Utume wetu mwema haukuwa kwenu katika maneno tu, ila ulitenda hata nguvu, ukawapo nayo Roho takatifu, mkapata pa kujishikizia sana; mwajua, tulivyokuwa kwenu kwa ajili yenu.
6
Nanyi mkatuiga sisi naye Bwana; mlikuwa na maumivu mengi, mkalipokea Neno kwa furaha, watu wapewayo na Roho takatifu.
7
Kwa hiyo wote wamtegemeao Mungu katika nchi ya Makedonia na ya Akea waliweza kujifundishia kwenu ninyi.
8
Kwani uvumi wa Neno la Bwana ulitoka kwenu, ukaenea Makedonia na Akea, lakini si huko tu, ila imejulikana waziwazi po pote, mnavyomtegemea Mungu. Kwa hiyo haitupasi sisi kuvisema mahali po pote,
9
kwani wenyewe huvisimuliana, mlivyotupokea, tulipoingia kwenu, nanyi mlivyomgeukia Mungu mkaviacha vinyago vya kutambikia, mpate kumtumikia Mungu aliye mwenye uzima na ukweli,
10
tena mnavyomgojea Mwana wake, atoke mbinguni; ni yeye Yesu, aliyemfufua katika wafu, naye ndiye atakayetuokoa katika makali yatakayokuja.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5