bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Thessalonians 3
1 Thessalonians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
1
Kwa hiyo hatukuweza kuvumilia tena, tukapendezwa kuachwa peke yetu huko Atene,
2
tukamtuma ndugu yetu Timoteo anayemtumikia Mungu na kuutangaza Utume mwema wa Kristo; tulimtuma, awashupaze ninyi na kuwatuliza mioyo kwa hivyo, mnavyomtegemea Mungu,
3
mtu asitikisike katika maumivu ya siku hizi; kwani mwajua wenyewe: jambo tulilowekewa, ni hilo.
4
Kwani hata hapo, tulipokuwa kwenu, tuliwafumbulia kwamba: Inatupasa kuumizwa; ndivyo vilivyotimia sasa, kama mnavyojua.
5
Kwa hiyo nami sikuweza kuvumilia tena, nikamtuma, nipate kutambua, kama mwamtegemea Mungu bado, au kama yule mwenye kujaribu amewajaribu, masumbuko yetu ya kwenu yakawa ya bure.
6
Lakini sasa Timoteo amefika kwetu kutoka kwenu, akatusimulia vema mambo mema, mnavyomtegemea Mungu, mnavyopendana, mnavyotukumbuka vema siku zote mkitunukia kutuona sisi, kama sisi tunavyotunukia kuwaona ninyi.
7
Kwa hayo, ndugu, tumetulizwa mioyo kwa ajili yenu katika mahangaiko na maumivu yetu yote, tuliposikia, mnavyomtegemea Mungu.
8
Kwani sasa tumerudi uzimani tena, ikiwa ninyi mmesimama penye Bwana.
9
Kwa shukrani gani, tutakazomtolea Mungu kwa ajili yenu, tutaweza kumlipa furaha zote, tulizozipata kwenu mbele yake yeye Mungu wetu?
10
Nasi twafuliza kuomba sanasana usiku na mchana, tupate kuonana nanyi uso kwa uso, tuweze kuziongeza nguvu zenu za kumtegemea Mungu, pakiwapo zilipokoseka.
11
Yeye Mungu aliye Baba yetu naye Bwana wetu Kristo na atuongoze njia ya kufika kwenu!
12
Ninyi Bwana awaongezee upendano, mfurikiwe nao, mpate kupendana ninyi kwa ninyi, kisha mwapende nao wote wengine, kama sisi nasi tunavyowapenda ninyi!
13
Hivyo mioyo yenu itashupaa, tena haitakosa kutakata kwa kuwa haina madoadoa, Mungu aliye Baba yetu akiitazama hapo, Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake wote.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5