bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Thessalonians 4
1 Thessalonians 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
*Pamesalia, ndugu, tuwahimize na kuwabembeleza, kwa hivyo, mlivyo wake Bwana Yesu, mfanye mwenendo uwapasao wa kumpendeza Mungu ulivyo.
2
Kwani mwayajua maagizo, tuliyowaagiza, kama tulivyoyapata kwake Bwana Yesu.
3
Kwani haya ndiyo, Mungu ayatakayo: mtakaswe, mwuepuke ugoni.
4
Kila mmoja wenu ajue kuuangalia mwili wake, uwepo ukitakata na kupata heshima iupasayo,
5
usivurugikane na tamaa na kijicho, kama wamizimu walivyofanya, wasiomjua Mungu!
6
Katika jambo hili mtu asiupite mpaka akimdanganya ndugu yake, kwani Bwana ndiye atakayeyalipizia hayo yote, kama tulivyowaambia kale na kuwashuhudia.
7
Kwani Mungu hakutuitia kuwa wenye uchafu, ila tuje, tutakaswe.
8
Basi, kwa hiyo mtu akiyatangua haya, hatangui ya mtu, ila yake Mungu aliyewapa ninyi Roho wake Mtakatifu, awakalie.
9
Kwa ajili ya upendano ninyi hampaswi na kuandikiwa neno, kwani ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.
10
Nanyi mnawafanyia hivi ndugu wote katika nchi yote ya Makedonia. Lakini twawaonya ninyi, ndugu, lifulizieni jambo hili!
11
Uchuchumieni utulivu, mpate kuyafuata mambo yenu wenyewe na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaagiza!
12
Sharti mfanye mwenendo uwafaliao wale watu wa nje, kwao msitake mtu wo wote wa kuwasaidia.*
13
*Lakini, ndugu, hatutaki, ninyi mkose kujua, mambo yao waliolala yalivyo, msione masikitiko kama wale wengine wasio na kingojeo.
14
Kwani tukiyategemea, ya kuwa Yesu alikufa, kisha akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu nao waliolala katika Yesu atawapeleka, wawe pamoja naye.
15
Kwani neno hili, tunalowaambia, ni neno lake Bwana kwamba: Sisi tunaoishi, tuliosazwa, mpaka Bwana atakapokuja, hatutawatangulia wale waliolala.
16
Kwani Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni papo hapo, wito utakapovumika, nayo sauti ya malaika mkuu itasikilika, hata baragumu la Mungu litalia. Ndipo, waliokufa katika Kristo watakapofufuka kwanza;
17
kisha sisi tuliosazwa, tutakaokuwa tu hai, tutapokonywa katika mawingu pamoja nao hao, tupate kukutana na Bwana angani. Hivyo tutakuwa pamoja na Bwana siku zote.
18
Tulizaneni mioyo ninyi kwa ninyi na kisimuliana maneno haya!*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5