bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Thessalonians 5
1 Thessalonians 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
1
Ndugu, hampaswi na kuandikiwa, kama itakuwa mwaka gani au siku gani, hayo yatakapokuwapo.
2
Kwani wenyewe mwajua sana: siku ya Bwana itafika, kama mwizi anavyokuja usiku.
3
Watakaposema: Pametengemana, pametulia, ndipo, watakapogunduliwa na mwangamizo, kama uchungu wa kuzaa unavyompata mwenye mimba; kwa hiyo hawataweza kukimbia.
4
Lakini ninyi, ndugu, hammo gizani, kwa hiyo siku ile hitawafumania kama mwizi.
5
Kwani ninyi wote ni wana wa mwanga na wana wa mchana; sisi hatu wa usiku, wala wa giza.
6
Kwa sababu hii tusilale usingizi, kama wale wengine wanavyolala usingizi, ila tukeshe na kulevuka!
7
Kwani wanaolala usingizi hulala usiku, nao wanaolewa hulewa usiku.
8
Lakini sisi tulio wa mchana tulevuke! Kisha tujivike mata: kumtegemea Mungu na kupendana kuwe kanzu zetu za chuma, nako kuungojea wokovu kuwe kofia zetu ngumu.
9
Kwani Mungu hakutuweka, tuishie kwa makali yake, ila alituweka, tuupate wokovu kwa kazi ya Bwana wetu Yesu Kristo
10
aliyekufa kwa ajili yetu sisi, tupate kuishi pamoja naye yeye, tukiwa tuko macho, au tukiwa tumelala usingizi.
11
Kwa hiyo mtulizane na kujengana kila mmoja na mwenzake, kama mnavyofanya!
12
Ndugu, twawaomba sana, mwajue wale wanaojisumbua kwenu ninyi wakiwasimamia, mkae naye Bwana, tena wakiwaonya.
13
Jipigieni sana kuwapa macheo na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao! Pataneni ninyi kwa ninyi!
14
*Lakini twawahimiza ninyi, ndugu: Waaonyeni wenye mambo ya ovyo tu, watulizeni wenye mioyo miepesi, wasaidieni wanyonge, wo wote waendeeni kwa uvumilivu!
15
Mwangalie, mtu asimlipe mwenziwe uovu kwa uovu! Ila siku zote myafuate yaliyo mema, myapatiane ninyi kwa ninyi, hata wengine wote!
16
Changamkeni siku zote!
17
Mwombeni Mungu pasipo kukoma!
18
Katika mambo yote toeni shukrani! Kwani haya ndiyo, Mungu ayatakayo, myafanye, kwa kuwa wake Kristo Yesu.
19
Roho msimzime!
20
Mafumbuo msiyabeze!
21
Ila yote yapambanueni, kisha lishikeni lililo jema!
22
Yote yaonekanayo kuwa mabaya yaepukeni!
23
Lakini yeye Mungu aliye mwenye utengemano awatakase ninyi nyote miili na mioyo, kwamba roho zenu zote nzima pamoja na mioyo na miili zilindwe, zikae pasipo doadoa lo lote, mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakaporudi!
24
Naye aliyewaita ni mwelekevu, naye ndiye atakayeyafanya.*
25
Ndugu, tuombeeni kwake Mungu!
26
Wasalimuni ndugu wote na kunoneana, kama watakatifu walivyozoea!
27
Nawaapisha ninyi kwa Bwana, barua hii isomewe ndugu wote.
28
Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie! Amin.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
All chapters:
1
2
3
4
5