bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Timothy 1
2 Timothy 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 2 →
1
Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, nikitangaze kiagio cha uzima uliomo mwake Kristo Yesu, nakuandikia barua, wewe Timoteo, mwanangu mpendwa.
2
Upole ukukalie na wema na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu, Bwana wetu!
3
Namshukuru Mungu, ninayemtambikia tangu siku za baba zangu kwa moyo utakatao kwa kujua mema tu. Nakukumbuka pasipo kukoma nikiomba usiku na mchana.
4
Nami nikiyakumbuka machozi yako, ninatunukia kukuona wewe, furaha zinifurikie.
5
Maana nakukumbuka moyoni, unavyomtegemea Mungu pasipo ujanja; kwanza bibi yako Loi alikukalia kumtegemea Mungu vivyo hivyo, kisha mama yako Eunike naye, lakini moyo wangu unajua, ya kuwa hata wewe unako.
6
Kwa sababu hii nakukumbusha, uyafuate yale mema yaliyomo mwako, uliyogawiwa hapo, nilipokubandikia mikono.
7
Kwani Mungu hakutupa Roho ya kutuogopesha, ila ya kututia nguvu na upendo tuonyeke.
8
Basi, usiingiwe na soni ya kumshuhudia Bwana wetu, hata mimi niliyefungwa kwa ajili yake! Ila ukiumizwa vibaya kwa ajili ya Utume mwema vumilia pamoja nami kwa nguvu za Mungu!
9
Maana ndiye aliyetuokoa, ndiye aliyetuitia kuwa watakatifu; naye hakutuitia kwa hivyo, matendo yetu yalivyo, ila kwa hiyovyo, alivyotaka mwenyewe toka kale kutugawia yale mema yaliyomo mwake Kristo Yesu; ni yayo hayo, tuliyolimbikiwa mbele ya mwanzo wa siku za kale.
10
Lakini siku za sasa yametufunikia hapo, mwokozi wetu Kristo Yesu alipotokea; ndiye aliyezitangua nguvu za kifo, kisha akatokeza mwangani uzima usioangamika, kama tulivyoambiwa na Utume mwema;
11
nami nikawekwa kuutangaza na kuutumikia na kuufundisha.
12
Kwa sababu yake nateseka hivyo, lakini sivionei soni, kwani namjua, nimtegemeaye. Tena ninalo shikizo hili la kwamba: Yuko na nguvu ya kulilinda limbiko langu, mpaka siku ile itakapotimia.
13
Uliyoyasikia kwangu mimi, shikamana nayo! Kwani ni kielezo cha kujifundishia yale maneno yatupayo uzima, tukimtegemea Kristo Yesu na kumpenda!
14
Hilo limbiko zuri sharti ulilinde kwa nguvu za Roho takatifu ikaayo ndani yetu sisi!
15
Neno lile nalijua, ya kuwa wote walioko Asia wameniacha; miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene.
16
Bwana awahurumie wao wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa kuwa amenipoza moyo mara nyingi; hakuwa na soni ya mafungo yangu,
17
ila alipofika Roma akajipingia kunitafuta, mpaka akiniona.
18
Bwana ampe kuona huruma kwake Bwana siku ile! Nayo yote, aliyonitimikia huko Efeso, wewe umeyatambua kuliko mimi.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4