bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Timothy 2
2 Timothy 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
1
Basi wewe mwanangu, ujipatie nguvu, tunazogawiwa tukiwa wake Kristo Yesu!
2
Nayo mambo, uliyoyasikia kwangu mbele yao wengi waliosikiliza, hayo uwalimbikishe watu welekevu watakaoweza kufundisha hata wengine.
3
Vumilia ukiteswa vibaya pamoja nami, kama inavyompasa askari mzuri wa Kristo Yesu!
4
Hakuna askari wa kwenda vitani anayejitia katika machumo ya pamba, ampendeze yule mwenye vita.
5
Lakini mtu angawa anashindana, hafungwi kilemba asiposhinda kikweli.
6
Mkulima ajisumbuaye na kulima imempasa kuyalimbua matunda.
7
Itambue maana yao, nisemayo! Kwani Bwana atakupa utambuzi katika mambo yote.
8
*Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa katika wafu, aliyezaliwa katika uzao wa Dawidi, kama nilivyoutangaza Utume mwema.
9
Kwa ajili yake nateseka vibaya, mpaka nikifungwa kama mwenye maovu, lakini Neno la Mungu halifungiki.
10
Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili yao waliochaguliwa, kwamba nao waupate wokovu uliomo mwake Kristo Yesu, wafike penye utukufu wa kale na kale.
11
Neno hili ni la kweli: Kama tumekufa pamoja naye;
12
kama twavumilia pamoja naye, tutatawala pamoja naye; kama tutakana kwamba: Hatu wake, naye atatukana sisi;
13
kama hatumtegemei, yeye hufuliza kuwa mwelekevu, kwani hawezi kujikana mwenyewe.*
14
Wakumbushe mambo hayo na kuwaonya mbele yake Mungu, wasibishane! Maana haifai kitu, huwapotoa tu wenye kusikiliza.
15
Jipingie kujitokeza kwa Mungu kuwa mfanya kazi aliye wa kweli, asiyefanya mambo yenye soni, anayelilinganisha vema neno la kweli, atakalogawia watu!
16
Lakini penye upuzi wa bure usio na maana uepuke! Kwani wako watakaoendesha mambo ya kumbeza Mungu,
17
nalo neno lao litaambukiza kama ukoma; miongoni mwao hao wamo Himeneo na Fileto
18
waliopotelewa nayo yaliyo ya kweli wakisema: Ufufuko umekwisha kuwapo. Ndivyo, walivyokosesha hata wengine, wasimtegemee Bwana tena.
19
Lakini msingi, Mungu aliouweka, uko, umeshupaa vivyo hivyo, hujulikana kwa muhuri yake, ni hii: Bwana huwatambua walio wake! Tena: Kila mwenye kulitambikia Jina la Bwana atenguke penye upotovu!
20
Katika nyumba kubwa hamna vyombo vya dhahabu au vya fedha tu, ila vimo hata vyombo vya miti na vya udongo; navyo vingine ni vya mapambo, vingine ni vya machafu.
21
Mtu akiwaepuka wale watu, asijichafue, atakuwa chombo cha pambo kilichotakaswa, naye mwenye nyumba atakitumia, maana kimefalia kazi zote zilizo njema.
22
Tamaa za ujana zikimbie, ukimbilie kupata wongofu na kumtegemea Mungu na kupendana na kupatana nao wote wanaomtambikia Bwana kwa mioyo itakatayo!
23
Lakini mabishano ya upuzi wa watu wasioonyeka yakatae! Jua, ya kuwa huleta magombano tu!
24
Lakini aliye mtumwa wa Bwana haimpasi kugombana, sharti awaendee wote kwa unyenyekevu akijua kuwafundisha, akivumilia wenye uovu.
25
Akiwa mpole hivyo ataweza kuwaonya wapingani nao, kama Mungu anawajutisha, wayatambue yalio ya kweli;
26
kisha watalevuka, wajinasue matanzini mwa Msengenyaji, ambaye walinaswa naye, wamfanyizie, ayatakayo yeye.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4