bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Timothy 4
2 Timothy 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
1
Namtaja Mungu naye Kristo Yesu atakayewahukumu wanaoishi hata waliokufa, awe shahidi, nikikuagiza haya: Kwa hivyo, atakavyotokea, ausimike ufalme wake,
2
litangaze Neno! Fuliza hivyo, pafaapo napo pasipofaa! Waonyeshe ubaya wao, wagombeze, wakanye ukiwaendea kna uvumilivu wote pamoja na kuwafundisha!
3
Kwani siku zinakuja, watakapoukataa ufundisho utupao uzima, ila kwa hivyo, watakavyozifuata tamaa zao wenyewe, watajitafutia wafunzi wengi wa kuwafundisha yapendezayo masikioni pao.
4
Nao watajigeuza, wasiyasikilize tena yaliyo ya kweli, wayageukie yalio masimulio tu.
5
*Lakini wewe levuka katika mambo yote! Vumilia ukiteswa vibaya! Fanya kazi ya mpiga mbiu njema! Utimize utumishi wako!
6
Kwani mimi pamenifikia, niwe ng'ombe ya tambiko, nayo siku yangu ya kufunguliwa kutoka ulimwenguni iko karibu.
7
Nimelishindania shindano zuri, nimeimaliza mbio, sikuacha kumtegemea Bwana.
8
Lisaalo ni kufungwa kilemba kipasacho waongofu, nilichowekewa nami Siku ile nitakipata kwake Bwana aliye mhukumu mwenye kweli; lakini si mimi tu atakayekipata, ila nao wote waliokuwa wamempenda, atokee waziwazi.*
9
Jikaze, ufike kwangu upesi!
10
Kwani Dema ameniacha, kwa kuyapenda mambo ya dunia hii akaenda zake Tesalonike. Kreske amekwenda zake Galatia, Tito amekwenda zake Dalmatia.
11
Luka peke yake yuko pamoja nami. Mchukue Marko, uje pamoja naye! Kwani hunitumikia vizuri sana.
12
Tikiko nalimtuma Efeso.
13
Utakapokuja ulete na lile joho gumu, nililoliacha huko Tiroa kwa Karpo! Vilete hata vile vitabu! Nivitakavyo sana, ni vile vya ngozi.
14
Alekisandro, yule mfua shaba amenifanyia maovu mengi; Bwana atamlipa, kama matendo yake yalivyo.
15
Hata wewe ujilinde kwa ajili ya mtu huyo, kwani ameyapinga sana maneno yetu.
16
Nilipojikania mara ya kwanza, hakuwapo hata mmoja aliyesimama upande wangu, wote waliniacha. Wasihesabiwe jambo hili!
17
Lakini Bwana alisimama upande wangu, akanipa nguvu, maana alitaka, ile mbiu itimizwe nami mimi, wamizimu wote wapate kuisikia. Nami nikaokolewa kinywani mwa simba.
18
Naye Bwana akaniokoa katika mambo mabaya yo yote, nipone, niingie katika ufalme wake wa mbinguni. Yeye atukuzwe siku zote kale na kale! Amin.
19
Nisalimie Puriska na Akila walio wa nyumbani mwa Onesifiro!
20
Erasto alisalia Korinto, Tirofimo nalimwacha mgonjwa Mileto
21
Jikaze, ufike, siku za kipupwe zitakapokuwa hazijatimia! Wanakusalimu Eubulo na Pude na Lino na Klaudia na ndugu wote.
22
Bwana awe na roho yako! Upole uwakalie ninyi! Amin.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
All chapters:
1
2
3
4