bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Timothy 3
2 Timothy 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 4 →
1
Lakini yatambue haya: siku za mwisho patakuwa na siku ngumu.
2
Kwani watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye choyo, wenye kujitutumua na kujikweza, wenye matusi, wasiwatii wazazi, wasishukuru, wasimche Mungu,
3
wasiwapende wenzao, wasitake kupatanishwa na mtu kwa kupenda usengenyaji, wasijikataze lo lote, wasionyeke, wasipende mema yo yote,
4
ila watakuwa wachongezi na wakorofi na wenye majivuno; kuzifuata tamaa za miili watakupenda kuliko kumfuata Mungu;
5
watajitendekeza kuwa wenye kumcha Mungu, lakini nguvu yake huipingia. Walio hivyo uwaepuke!
6
Kwani wenzao ndio wale wanaonyemelea nyumbani mwa watu, watongoze wanawake wanyonge waliolemewa na makosa, wakiongozwa na tamaa nyingi;
7
hao hufundishwa toka kale, lakini hapana, watakapoweza kuufikia utambuzi wa kweli.
8
Kama Yane na Yambure waliombisha Mose, ndivyo, hata hao wanavyoyabisha yalio ya kweli; hufanana nao wenye wazimu, wakajulika kuwa wenye kumtegemea Mungu bure tu.
9
Lakini hawataendelea sana, kwani upumbavu wao utawatokea wote waziwazi, kama hata upumbavu wao wale ulivyojulika.
10
Lakini wewe umeufuata ufundisho wangu na mwenendo wangu na mawazo yangu na njia yangu ya kumtegemea Mungu na utulivu wangu na upendo wangu na uvumilivu wangu,
11
hata mafukuzo na mateso yangu, niliyoyapata huko Antiokia na Ikonio na Listra. Nami niliyavumilia hayo mafukuzo yote, naye Bwana akaniokoa katika yote.
12
Nao wote wanaotaka kuishi na kumcha Mungu kwa kuwa wake Kristo Yesu sharti wapate mafukuzo.
13
Lakini watu walio wabaya na wadanganyi wataendelea, wajifikishe palipo pabaya; hupoteza watu, tena hupotezwa wenyewe.
14
*Lakini wewe ukae na kuyashika yale, uliyofundishwa, uliyoyatambua kwamba: Ndiyo ya kweli, maana unajua, waliokufundisha walivyo.
15
Tena kwa sababu umeyajua Maandiko matakatifu tangu utoto wako, haya yanaweza kukuerevusha, uokoke kwa kumtegemea Kristo Yesu.
16
Kwani kila neno la Maandiko, mtu aliloambiwa na Mungu, linafaa, litufundishe, lituonyeshe ubaya wetu, liitulize mioyo yetu, lituonye, tupate wongofu;
17
ndivyo, anavyotengenezewa mtu wa Kimungu ajikazaye kufanya kazi njema zo zote.*
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4