bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezra 1
Ezra 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 2 →
1
Katika mwaka wa kwanza wa Kiro, mfalme wa Wapersia, ndipo, lilipotimia neno la Bwana, alilolisema kinywani mwa Yeremia, maana Bwana akaiamsha roho yake Kiro, mfalme wa Wapersia, akatangaza mbiu katika ufalme wake wote kwa vinywa vya watu na kwa barua kwamba:
2
Hivi ndivyo, anavyosema Kiro, mfalme wa Wapersia: Ufalme wote wa nchi hii amenipa Bwana Mungu wa mbinguni, naye mwenyewe akaniagiza kumjengea Nyumba kule Yerusalemu katika nchi ya Yuda.
3
Ye yote wa kwenu aliye wa ukoo wake Mungu wake awe naye, na apande kwenda Yerusalemu katika nchi ya Yuda kuijenga Nyumba ya Bwana Mungu wa Isiraeli. Yeye akaaye Yerusalemu ni Mungu.
4
Tena kila atakayesalia mahali po pote, anapokaa ugenini, watu wa mahali pale sharti wamsaidie kwa kumpa fedha na dhahabu na vyombo na nyama wa kufuga pamoja na vipaji vingine, wanavyovitaka wenyewe vya kuitolea Nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu.
5
Ndipo, wao waliokuwa vichwa vya milango ya Yuda na ya Benyamini pamoja na watambikaji na Walawi walioamshwa roho zao na Mungu wakaondoka kwenda kuijenga Nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu.
6
Nao waliokaa na kuwazunguka wakaitia mikono yao nguvu kwa kuwapa fedha na dhahabu na vyombo na nyama wa kufuga na vitu vyenye kima, tena vipaji vyote, walivyovitoa wenyewe vya tambiko.
7
Naye mfalme Kiro akavitoa vyombo vyote vya Nyumba ya Bwana, Nebukadinesari alivyovitoa Yerusalemu na kuvitia jumbani mwake.
8
Hivyo Kiro, mfalme wa Wapersia, akavitoa na kuvitia mikononi mwa mtunza malimbiko Mitiridati, naye akavihesabu alipompa Sesebasari, mkuu wa Wayuda.
9
Hii ndiyo hesabu yao: sinia za dhahabu 30, sinia za fedha 1000, visu 29;
10
vinyweo vya dhahabu 30, vinyweo vya fedha vya namna ya pili 410, vyombo vingine 1000.
11
Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa 5400. Hivi vyote Sesebasari alikwenda navyo, wale waliotekwa na kuhamishwa walipotoka Babeli kwenda kupanda Yerusalemu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10