bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezra 6
Ezra 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 7 →
1
Ndipo, mfalme Dario alipotoa amri, wakachunguza nyumbani mwenye vitabu, mlimowekwa navyo vilimbiko vya huko Babeli.
2
Kisha kikaoneka kizingo cha karatasi katika mji wa Ahimeta katika nchi ya Media; ndimo, nalo jumba la mfalme lilimokuwa. Ile karatasi ilikuwa imeandikwa: Ukumbusho.
3
Kwamba: Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Kiro huyu mfalme Kiro akatoa amri, Nyumba ya Mungu huko Yerusalemu na ijengwe kuwa mahali, watakapotoa ng'ombe za tambiko, misingi yake itengenezwe kuwa na nguvu; urefu wake uwe mikono sitini, nao upana wake uwe mikono sitini.
4
Waweke masafu matatu ya mawe makubwa ya kuchonga, tena safu moja la mbao mpya; nazo fedha za kulipa wapewe, zitoke nyumbani mwa mfalme.
5
Navyo vyombo vya Nyumba ya Mungu vya dhahabu na vya fedha, Nebukadinesari alivyovitoa Nyumbani mle Yerusalemu na kuvipeleka Babeli, sharti virudishwe, vije Nyumbani mwa Yerusalemu kila kimoja mahali pake na kuwekwa mle Nyumbani mwa Mungu.
6
Sasa wewe Tatinai, mtawala nchi zilizoko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, na Setari-Bozinai pamoja na wenzako Waafarsaki walioko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, jitengeni, msifike huko!
7
Waacheni, kazi za Nyumba hii ya Mungu ziendelee, mtawala nchi wa Wayuda na wazee wa Wayuda waijenge Nyumba hiyo ya Mungu hapo, ilipokuwa!
8
Mimi natoa amri, ya kwamba msaidiane na hao wazee katika kuijenga Nyumba hiyo ya Mungu, mkifanya bidii, mpate kutoa mali za mfalme zitokazo katika kodi za nchi zilizoko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, watu hao wapewe kila mara fedha za kuzilipa hizo hazi, wasizuiliwe.
9
Nayo mengine wanayopaswa nayo, kama madume ya ndama na madume ya kondoo na wana kondoo wa kuwa ng'ombe za tambiko za Mungu wa mbingu, tena ngano na chumvi na mvinyo na mafuta, kama watambikaji walioko Yerusalemu wanavyovitaka, sharti wapewe siku kwa siku, visikoseke,
10
wapate kumtolea mungu wa Mbingu minuko mizuri na kuwaombea wafalme na wana wao, wawe wenye uzima.
11
Tena ninatoa amri kwamba: Kila mtu atakayeligeuza neno hili nyumbani mwake itolewe nguzo, isimikwe, kisha mwenyewe atundikwe humo, nayo nyumba yake igeuzwe kuwa kifusi kwa ajili hiyo.
12
Naye Mungu atakayelikalisha Jina lake mle na awabwage chini wafalme wote na watu wote watakaokunjua mikono yao, waligeuze neno hili, waiharibu Nyumba hiyo ya Mungu iliyomo Yerusalemu. Mimi Dario nimeitoa amri hii, sharti ifanyizwe pasipo kuikosea.
13
Kwa hiyo Tatinai, mtawala nchi zilizoko ng'ambo ya huku ya jito kubwa, na Setari-Bozinai na wenzao wakafanya sawasawa kabisa, kama mfalme Dario alivyowaagiza katika hiyo barua.
14
Nao wazee wa Wayuda wakaendelea kujenga, wakafanikiwa, kama wafumbuaji Hagai na Zakaria, mwana wa Ido, walivyowaambia kwa ufumbuaji wao: wakajenga, hata wakamaliza kwa amri yake Mungu wa Isiraeli na kwa amri za Kiro na za Dario na za Artasasta, wafalme wa Wapersia.
15
Nyumba hii ikamalizika siku ya tatu ya mwezi wa Adari, nao ule mwaka ulikuwa wa sita wa ufalme wa mfalme Dario.
16
Ndipo, wana wa Isiraeli, watambikaji na Walawi nao wale wengine waliotoka kwenye kutekwa walipoieua Nyumba hii ya Mungu kwa furaha.
17
Hapo walipoieua Nyumba hii ya Mungu wakatoa ng'ombe 100 na madume ya kondoo 200 na wana kondoo 400 kuwa ng'ombe za tambiko, tena madume 12 ya mbuzi kwa hesabu ya mashina ya Isiraeli kuwa ng'ombe za tambiko za weuo wa ukoo mzima wa Isiraeli.
18
Kisha wakaweka watambikaji kwa vyama vyao nao Walawi kwa kura zao, walizopigiwa, wamtumikie Mungu mle Yerusalemu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mose.
19
Kisha wao waliotoka kwenye kutekwa wakafanya sikukuu ya Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
20
Kwani watambikaji na Walawi walijitakasa pamoja, wakatakata wote pia, wakawachinjia kondoo wa Pasaka wote waliotoka kwenye kutekwa nao ndugu zao watambikaji nao wao wenyewe.
21
Wana wa Isiraeli waliorudi kwenye kutekwa wakaila pamoja nao waliotaka kumfuata Bwana Mungu wa Isiraeli, waliojitenga, wasijichafue kwa wamizimu wenzao waliokaa kwao katika nchi hii.
22
Wakaifanya hiyo sikukuu ya Mikate isiyochachwa siku saba na kufurahi, kwani Bwana aliwafurahisha kwa kuugeuza moyo wa mfalme wa Asuri, uwaelekee, aishupaze mikono yao katika kazi ya Nyumba ya Mungu aliye Mungu wa Isiraeli.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10