bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nehemiah 1
Nehemiah 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 2 →
1
Haya ni mambo ya Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisilewu wa mwaka wa ishirini, nilipokuwa Susani mlimo na jumba la mfalme.
2
Ndipo, alipokuja Hanani, mmoja wao ndugu zangu, pamoja na watu waliotoka Yuda. Nikawauliza habari za Wayuda waliopona, ndio wale waliosalia, wenzao walipohamishwa, na habari za Yerusalemu.
3
Wakaniambia: Yale masao ya watu waliosalia kule jimboni, wenzao walipohamishwa, wamo katika mabaya mengi yawatiayo soni: boma la Yerusalemu lingaliko limebomolewa, nayo malango yake yako vivyo hivyo, yalivyoteketezwa kwa moto.
4
Nilipoyasikia maneno haya, nikakaa siku zile na kulia machozi kwa kusikitika, nikawa mikifunga mfungo na kumwomba Mungu wa mbinguni,
5
nikasema: E. Bwana Mungu wa mbinguni, u Mungu mkubwa, unaogopesha, lakini wao wakupendao na kuyashika maagizo yako unawatimilizia Agano lako na upole wako.
6
Sasa sikio lako na liwe limetegwa, nayo macho yako na yawe wazi, uyasikilize malalamiko ya mtumwa wako, nikulalamikiayo mimi leo mchana na usiku kwa ajili ya wana wa Isiraeli walio watumwa wako, nikikutolea makosa yao wana wa Isiraeli, tuliyokukosea, mimi nami nao wa mlango wa baba yangu tumekosa.
7
Tumekufanyizia maovu mengi, hatukuyashika maagizo, wala maongozi, wala maamuzi yako, uliyomwagiza mtumishi wako Mose.
8
Likumbuke lile neno, ulilomwagiza mtumishi wako Mose la kwamba: Mtakapoyavunja maagano, mimi nitawatapanya kwenye makabila yote;
9
lakini mtakaporudi kwangu na kuyashika maagizo yangu, myafanye, nitawakusanya, ijapo mwe mmekimbizwa mpaka kwenye mapeo ya mbingu; huko nako nitawatoa na kuwapeleka mahali hapo, nilipopachagua, pawe pa kulikalishia Jina langu.
10
Nao ndio watumwa wako na ukoo wako, uliowakomboa kwa nguvu zako kuu na kwa mkono wako unaoshupaa.
11
E Bwana, sasa sikio lako na liwe limetegewa maombo ya mtumwa wako na malalamiko ya watumwa wako wanaopendezwa na kulicha Jina lako! Umfanikishe leo mtumwa wako na kumhurumia machoni pa mtu huyu! Kwani nilikuwa mtunza vinywaji kwake mfalme.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13