bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nehemiah 7
Nehemiah 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
1
Ikawa, boma lilipokwisha kujengwa, nikatia milango, wakawekwa walinda malango na waimbaji na Walawi,
2
nikamwagiza ndugu yangu Hanani na Hanania, mkuu wa boma, kushika amri humu Yerusalemu, kwani huyu alikuwa mtu mwelekevu mwenye kumcha Mungu kuliko wengine wengi.
3
Nikawaambia: Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe, mpaka jua liwake na nguvu; tena walinzi wakingali wanasimama, malango yafungwe na kutiwa makomeo. Tena mweke wenyeji wa Yerusalemu kuwa walinzi kila mtu na zamu yake ya kulinda hapo panapoielekea nyumba yake.
4
Lakini mji ulikuwa mpana pande zote na mkubwa, lakini watu waliomo walikuwa wachache, hata nyumba mpya hazikujengwa.
5
Mungu akanitia moyoni, niwakusanye wakuu wa miji na watawalaji nao watu, waandikwe milango yao. Nikaona chuo kilichoandikwa udugu wao walionza kurudi na kupanda huku, nikaona yameandikwa haya:
6
Hawa ndio watu waliokaa majimboni waliporudi kutoka mafungoni kwenye kutekwa; ndio wao, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliowateka na kuwahamisha, nao wakapata kurudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake.
7
Walikuja pamoja nao Zerubabeli, Yesua, Nahemia, Azaria, Ramia, Nehamani, Mordekai, Bilsani, Misipereti, Bigwai, Nehumu na Baana. Hesabu ya waume wa Waisiraeli ni hii:
8
Wana wa Parosi 2172;
9
wana wa Sefatia 372;
10
wana wa Ara 652;
11
wana wa Pahati-Moabu, ndio wana wa Yesua na wa Yoabu, 2818;
12
wana wa Elamu 1254;
13
wana wa Zatu 845;
14
wana za Zakai 760;
15
wana wa Binui 648;
16
wana wa Bebai 628;
17
wana wa Azgadi 2322;
18
wana wa Adonikamu 667;
19
wana wa Bigwai 2067;
20
wana wa Adini 655;
21
wana wa Ateri walio wa Hizikia 98;
22
wana wa Hasumu 328;
23
wana wa Besai 324;
24
wana wa Harifu 112;
25
wana wa Gibeoni 95;
26
waume wa Beti-Lehemu na wa Netofa 188;
27
waume wa Anatoti 128;
28
waume wa Beti-Azimaweti 42;
29
waume wa Kiriati-Yearimu, wa Kefira na wa Beroti 743;
30
waume wa Rama na wa Geba 621;
31
waume wa Mikimasi 122;
32
waume wa Beteli na wa Ai 123;
33
waume wa Nebo wa pili 52;
34
wana wa Elamu wa pili 1254;
35
wana wa Harimu 320;
36
wana wa Yeriko 345;
37
wana wa Lodi, wa Hadidi na wa Ono 721;
38
wana wa Senaa 3930.
39
Watambikaji walikuwa hawa: wana wa Yedaya wa mlango wa Yesua 973;
40
wana wa Imeri 1052;
41
wana wa Pashuri 1247;
42
wana wa Harimu 1017.
43
Walawi walikuwa hawa: wana wa Yesua wa mlango wa Kadimieli na wana wa Hodawia 74.
44
Waimbaji walikuwa wana wa Asafu 148.
45
Walinda malango walikuwa wana wa Salumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Sobai, watu 138.
46
Watumishi wa Nyumbani mwa Mungu walikuwa hawa: wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaoti,
47
wana wa Kerosi, wana wa Sia, wana wa Padoni,
48
wana wa Lebana, wana wa Hagada, wana wa Salmai,
49
wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari,
50
wana wa Raya, wana wa Resini, wana wa Nekoda,
51
wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea;
52
wana wa Besai, wana wa Munimu, wana wa Nefisisimu,
53
wana wa Bakibuki, wana wa Hakufa, wana wa Harihuri;
54
wana wa Basiliti, wana wa Mehida, wana wa Harsa;
55
wana wa Barkosi; wana wa Sisera, wana wa Tema;
56
wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
57
Wana wa watumwa wa Salomo walikuwa hawa: wana wa Sotai, wana wa Sofereti, wana wa Perida,
58
wana wa Yala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli,
59
wana wa Sefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereti-Hasebaimu, wana wa Amoni.
60
Watumishi wa Nyumbani mwa Mungu na wana wa watumwa wake Salomo wote pamoja walikuwa 392.
61
Nao hawa ndio waliopanda toka Teli-Mela, Teli-Harsa, Kerubu-Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuijulisha milango ya baba zao, wala vizazi vyao, kama ndio Waisiraeli:
62
wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda; nao walikuwa watu 642.
63
Tena kwao watambikaji: wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai aliyechukua mmoja wao binti Barzilai wa Gileadi, awe mkewe, kwa hiyo aliitwa kwa jina lao.
64
Hawa walikitafuta kitabu chao cha udugu wao, lakini hawakukiona, kwa hiyo wakakatazwa utambikaji.
65
Mtawala nchi akawaambia: Msile kabisa vyakula vitokavyo Patakatifu Penyewe, mpaka atakapoondokea mtambikaji mwenye Urimu na Tumimu (Mwanga na Kweli).
66
Huo mkutano wote pamoja walikuwa watu 42360,
67
pasipo watumwa na vijakazi wao, nao walikuwa 7337; tena walikuwako waimbaji wa kiume na wa kike 245.
68
Farasi wao walikuwa 736, nyumbu wao 245,
69
ngamia 435, tena punda 6720.
70
Wakuu wengine wa milango wakatoa vipaji vya kufanyia hizo kazi za jengo: mtawala nchi alitoa na kutia katika kilimbiko: vipande vya dhahabu vilivyoitwa Dariko 1000, ndio shilingi kama 40000, na vyano 50 na mavazi ya watambikaji 530.
71
Nao wakuu wa milango wengine wakatoa na kutia katika kilimbiko cha jengo: vipande vya dhahabu vilivoitwa Dariko 20000, ndio shilingi kama 800000, na vipande vya fedha vilivyoitwa Mane 2200, ndio shilingi kama 440000.
72
Nao watu wengine wakatoa Dariko za dhahabu 20000, ndio shilingi kama 800000, na Mane za fedha 2000, ndio shilingi kama 400000 na mavazi ya watambikaji 67.
73
Kisha watambikaji na Walawi na walinda malango na waimbaji nao watu wengine na watumishi wa Nyumbani mwa Mungu nao Waisiraeli wote wakakaa katika miji yao. Mwezi wa saba ulipofika, wana wa Isiraeli walikuwamo bado mijini mwao.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13