bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nehemiah 2
Nehemiah 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 3 →
1
Ikawa katika mwezi wa Nisani wa mwaka wa ishirini wa mfalme Artasasta; hapo, mvinyo ilipowekwa mbele yake, nikaichukua hiyo mvinyo, nikampa mfalme; lakini mpaka hapo sijawa nikinuna mbele yake.
2
Mfalme akaniuliza: Mbona uso wako unanuna, ukiwa huugui? Hili si jingine, ila ni sikitiko la moyo. Ndipo, nilipoingiwa na woga mwingi sana,
3
nikamjibu mfalme: Mfalme na awe mwenye uzima kale na kale! Je? Uso wangu usinune, mji ulio na makaburi ya baba zangu ukiwa umebomoka, nayo malango yake yakiwa yameteketezwa kwa moto?
4
Mfalme akaniuliza: Sasa wewe unatakaje? Ndipo, nilipomwomba Mungu wa mbinguni,
5
nikamwambia mfalme: Vikiwa vema machoni pako, mfalme, mtumwa wako naye akiwa mwema machoni pako, nitume, niende katika nchi ya Yuda mle mjini mlimo na makaburi ya baba zangu, miujenge!
6
Mfalme akaniuliza, naye mkewe alikuwa amekaa kando yake, kwamba: Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Utarudi lini? Basi, mfalme akaviona kuwa vema, akanituma, nami nikaagana naye siku za kurudi.
7
Kisha nikamwambia mfalme: Vikiwa vema kwake mfalme, na wanipe barua za kuwapelekea wenye amri walioko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, waniache, nipite, mpaka nitakapofika Yuda.
8
Tena barua kwa Asafu, mtunza miitu ya mfalme, anipe miti ya kutengeneza nguzo za malango ya boma lililoko penye hiyo Nyumba, nayo ya ukuta wa mji na ya nyumba yangu, nitakamoingia. Mfalme akanipa, kwa kuwa mkono wa Mungu wangu ulio mwema ulikuwa na mimi.
9
Nilipofika kwao wenye amri ng'ambo ya huku ya jito kubwa, nikawapa zile barua za mfalme. Tena mfalme alikuwa amenipa hata wakuu wenye vikosi vya askari nao wapanda farasi.
10
Sanibalati wa Horoni na mtumishi Tobia wa Waamoni walipoyasikia haya, wakakasirika sanasana, ya kuwa amekuja mtu aliyetaka kuwatafutia wana wa Isiraeli mema.
11
Nilipofika Yerusalemu nikakaa huko siku tatu.
12
Kisha nikainuka usiku mimi na watu wachache, niliokuwa nao; lakini hakuwako mtu, niliyemwambia Mungu wangu aliyonitia moyoni, niyafanyize Yerusalemu, hata nyama sikuwa naye, isipokuwa yule, niliyempanda.
13
Nikatoka usiku huo katika lango la Bondeni, nikashika njia ya kwenda penye kisima cha Joka na penye lango la Jaani, nikawa nikizichungulia kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa, nayo malango yaliyokuwa yameliwa na moto.
14
Nikaendelea, nikafika penye lango la Jicho la Maji, hata penye ziwa la mfalme, lakini nyama, niliyempanda, hakuona mahali pa kupitia.
15
Ndipo, nilipokwea katika bonde la kijito usiku uleule, nikawa nikiuchungulia ukuta; kisha nikarudi, nikafika tena kwenye lango la Bondeni, nikarudi nyumbani.
16
Lakini wakuu hawakujua, wala nilikokwenda, wala niliyoyafanya; nami mpaka hapo sikuwaambia Wayuda neno lo lote, wala watambikaji, wala wakuu wa mji, wala watawalaji, wala wao wengine, niliowatakia kazi.
17
Nikawaambia: Mnayaona haya mabaya yaliyotupata, ya kuwa Yerusalemu ni mabomoko, nayo malango yake yameteketezwa kwa moto. Haya! Njoni, na tulijenge boma la Yerusalemu, tusiendelee kutukanwa!
18
Nikawasimulia, mkono wa Mungu ulio mwema ulivyonisaidia, nayo yale maneno, mfalme aliyoniambia. Ndipo, walipoitikia kwamba: Na tuinuke, tujenge! Nayo mikono yao wakaishupaza kufanya kazi njema.
19
Lakini Sanibalati wa Horoni na mtumishi Tobia wa Waamoni na Mwarabu Gesemu walipoyasikia, wakatucheka na kutubeza wakisema: Hii kazi yenu, mnayoifanya, ni ya nini? Mwataka kumkataa mfalme na kuacha kumtii?
20
Nikawajibu neno nikiwaambia: Mungu wa mbinguni atatupa kuimaliza kazi hii; sisi tulio watumwa wake tutainuka, tujenge. Lakini ninyi hamna fungu humu Yerusalemu wala cho chote kilicho chenu wala ukumbusho tu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13