bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Galatians 1
Galatians 1
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 2 →
1
PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),
2
na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia,
3
Neema iwe kweuu, na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo,
4
aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:
5
ambae ana utukufu milele na milele, Amin.
6
Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha hivi upesi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo,
7
mkageukia injili ya namna nyingine; wala si nyingine. Lakini wapo watu wawataabishao na watakao kuigeuza injili ya Kristo.
8
Lakini sisi au malaika wa mbinguni tukiwakhubiri ninyi injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.
9
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awae yote akiwakhubiri injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.
10
Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
11
Kwa maana injili biyo niliyowakhubiri nawajulisha, ndugu, ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.
12
Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.
13
Maana mmesikia khabari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi nikaliharibu,
14
nami nalitangulia katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kushika mapokeo ya baba zangu.
15
Lakini Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,
16
alipoona vema kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, illi niwakhubiri mataifa khabari zake, marra sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu,
17
wala sikupanda kwenda Yerusalemi kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nalikwenda zangu Arabuni nikarudi teua Dameski.
18
Kiisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemi illi nionaue na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano.
19
Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana.
20
Na bayo ninayowaandikieni, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uwongo.
21
Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia.
22
Lakini sikujulika uso wangu na makanisa ya Yahudi yaliyo katika Kristo;
23
ilia wamesikia tu ya kwamba yeye aliyetuudhi kwanza sasa anaikhubiri imani ile aliyoiharibu zamani.
24
Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6