bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Galatians 5
Galatians 5
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
1
KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.
2
Fahamuni, mimi Paolo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.
3
Tena namshuhudia killa mtu atahiriwae, kwamba ni wajibu wake kuitimiza sharia yote.
4
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.
5
Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la wema kwa njia ya imani.
6
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
7
Mlikuwa mkipiga mbio vizuri: ni nani aliyewazuia msiitii kweli?
8
Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye aliyewaita.
9
Chachu kidogo huchachua donge nzima.
10
Nina matumaini kwenu katika Bwana, kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anaewafadhaisha atachukua hukumu yake awae yote.
11
Na mimi, ndugu, ikiwa ninakhubiri khabari ya kutahiriwa, mbona ningali nikiudhiwa? Hapo kwazo la msaiaba limebatilika.
12
Ningependa hawo wanaowatieni mashaka wangejikata nafsi zao.
13
Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.
14
Maana sharia yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
15
Lakini mkiumana na kulana angalieni msije mkaangamizana.
16
Nasema, Enendeni kwa Roho, nanyi hamtatimiza tamaa za mwili.
17
Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka.
18
Lakini nikiongozwa na Roho, hunpo chini ya sharia.
19
Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki,
20
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,
21
husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu.
22
Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23
upole, kiasi; juu ya mambo ya jinsi hii hapana sharia.
24
Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.
25
Tukiisbi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
26
Tusijisifu burre, tukichokozana na kuhusudiana.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6