bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Galatians 6
Galatians 6
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
1
NDUGU, mtu ajapogbafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrudini mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako nsijaribiwe wewe mwenyewe.
2
Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sharia ya Kristo.
3
Maana mtu akijiona kuwa kitu, nae si kitu, ajidanganya nafsi yake.
4
Lakini killa mtu aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakuwa na sababu ya kujisifu kwa nafsi yake tu, wala si kwa kujilinganislia na mwenzake.
5
Maana killa mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.
6
Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.
7
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8
Maana yeye apandae kwa mwili wake, katika mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandae kwa Roho, katika Roho atavima uzima wa milele.
9
Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.
10
Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.
11
Tazameni kwa harufi gani kubwa nimewaandikieni kwa mkono wangu mimi mwenyewe.
12
Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mwili, ndio wanaokushurutisheni kutahiriwa: wasiudhiwe tu kwa ajili ya msalaba wa Kristo.
13
Kwa maana hatta wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sharia; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kujisifia miili yenu.
14
Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
15
Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.
16
Na wote watakaoiendea kanuni hii, amani kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.
17
Tangu sasa mtu asinitie taabu; kwa maana ninachiukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
18
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amin.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
All chapters:
1
2
3
4
5
6