bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Galatians 4
Galatians 4
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
1
LAKINI nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ajapokuwa bwana wa yote;
2
bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hatta muhulla uliokwisha kuamriwa na baba.
3
Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.
4
Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,
5
illi awakomboe waliokuwa chini ya sharia, tupate kupokea hali ya wana.
6
Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.
7
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali mwana; na kama u mwana, bassi, u mrithi wa Mungu kwa Kristo.
8
Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkujua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.
9
Bali sasa, mkiisha kumjua Mungu, ya nini kurejea tena kwa mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge na yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena.
10
Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.
11
Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha burre kwenu.
12
Nakusihini, ndugu, mwe kama mimi, maana mimi kama ninyi. Hamkunidhulumu neno.
13
Lakini mwajua ya kuwa naliwakhubiri Injili marra ya kwanza kwa sababu ya ndhaifu wa mwili;
14
na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.
15
Ku wapi, bassi, kule kujiita kheri? Maana nawashuhudia, kwamba, kama ingaliwezekana, mngaliugʼoa macho yenu, mkanipa mimi.
16
Bassi, je! nimekuwa adui wenu kwa sababu nawa ambieni yaliyo kweli?
17
Wao wawaonea uinyi shauku lakini si kwa vema bali wanataka kuwafungia mlango illi ninyi mwaonee wao shauku.
18
Na ni vyema kuonewa shauku katika neno jema siku zote, wala si wakati nikiwapo mimi tu.
19
Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.
20
Naam, ningependa kuwa pamoja nanyi sasa, na kuigeuza santi yangu; maana nawaonea maashaka.
21
Niambieni, ninyi ninaotaka kuwa chini ya sharia, hamwisikii torati?
22
Kwa maana, imeandikwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.
23
Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.
24
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio maagano mawili, moja toka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ndio Hajir.
25
Maana Hajir ni mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemi wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto wake.
26
Bali Yerusalemi wa juu ni mwungwana, ndio mama yetu sisi.
27
Kwa maana imeandikwa, Fanya furaha, tassa usiyezaa; Paaza sauti, ukalie, wewe usiye na utungu; Kwa sababu watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko wake aliye na mume.
28
Sisi, ndugu, kama Isaak, tu watoto wa ahadi.
29
Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alimwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, vivyo hivyo na sasa.
30
Lakini lanenani Andiko? Mtupe nje mjakazi na mwana wake, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.
31
Kwa hiyo, ndugu, sisi si watoto wa mjakazi, hali wake aliye mwungwana.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6