bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Psalms 106
Psalms 106
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 105
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 107 →
1
Haleluya! Msifuni Mwenyezi-Mungu! Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele!
2
Ni nani awezaye kutaja matendo ya Mwenyezi-Mungu? Ni nani awezaye kumsifu kama anavyostahili?
3
Heri wale wanaotekeleza haki, wanaotenda daima mambo yaliyo sawa.
4
Unikumbuke ee Mwenyezi-Mungu unapowafadhili watu wako; unisaidie wakati unapowaokoa;
5
ili niweze kuona fanaka ya wateule wako, nipate kufurahia furaha ya taifa lako, na kuona fahari pamoja na watu wako.
6
Tumetenda dhambi sisi na wazee wetu; tumetenda maovu, tumefanya mabaya.
7
Wazee wetu walipokuwa Misri, hawakujali matendo ya ajabu ya Mungu; hawakukumbuka wingi wa fadhili zake, bali walimwasi kando ya bahari ya Shamu.
8
Hata hivyo Mungu aliwaokoa kama alivyoahidi, ili aoneshe nguvu yake kuu.
9
Aliikemea bahari ya Shamu ikakauka; akawapitisha humo kama katika nchi kavu.
10
Aliwaokoa mikononi mwa waliowachukia; aliwaokoa kutoka kwa nguvu za maadui zao.
11
Maji ya bahari yaliwafunika maadui zao; wala hakusalia hata mmoja wao.
12
Hapo watu wake wakaamini maneno yake, wakamwimbia tenzi za sifa yake.
13
Lakini mara walisahau matendo yake, wakaacha kutegemea shauri lake.
14
Walijawa na tamaa kubwa kule jangwani, wakamjaribu Mungu kule nyikani.
15
Naye akawapa kile walichoomba, lakini akapeleka maradhi mabaya kati yao.
16
Kule kambini walimwonea wivu Mose, na Aroni mtumishi mtakatifu wa Mwenyezi-Mungu.
17
Ndipo ardhi ikafunguka ikammeza Dathani, na kumzika Abiramu na kundi lake lote;
18
moto ukawatokea wafuasi wao, ukawateketeza watu hao waovu.
19
Walitengeneza ndama wa dhahabu kule Horebu, wakaiabudu sanamu hiyo ya kusubu;
20
waliubadilisha utukufu wa Mungu, kwa sanamu ya mnyama ambaye hula nyasi.
21
Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyetenda mambo makuu nchini Misri,
22
maajabu katika nchi hiyo ya Hamu, na mambo ya kutisha katika bahari ya Shamu.
23
Mungu alisema atawaangamiza watu wake, ila tu Mose mteule wake aliingilia kati, akaizuia hasira yake isiwaangamize.
24
Kisha wakaidharau nchi ile ya kupendeza, kwa sababu hawakuwa na imani na ahadi ya Mungu.
25
Walinungunika mahemani mwao, wala hawakumsikiliza Mwenyezi-Mungu.
26
Hivyo Mungu akainua mkono akaapa kwamba atawaangamizia jangwani;
27
atawatawanya wazawa wao kati ya watu, na kuwasambaza duniani kote.
28
Kisha wakajiunga kumwabudu Baali kule Peori, wakala tambiko zilizotambikiwa mizimu.
29
Waliichochea hasira ya Mwenyezi-Mungu kwa matendo yao, maradhi mabaya yakazuka kati yao.
30
Lakini Finehasi akasimama kufanya malipizi, na yale maradhi yakakoma.
31
Jambo hilo lakumbukwa kwa heshima yake, tangu wakati huo na nyakati zote.
32
Walimkasirisha Mungu penye maji ya Meriba, Mose akapata taabu kwa ajili yao.
33
Walimtia Mose uchungu rohoni, hata akasema maneno bila kufikiri.
34
Hawakuwaua watu wa mataifa mengine kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru.
35
Bali walijumuika na watu wa mataifa, wakajifunza kutenda mambo yao.
36
Waliabudu sanamu za miungu yao, nazo zikawa mtego wa kuwaangamiza.
37
Waliwaua watoto wao wa kiume na wa kike, wakawatoa tambiko kwa pepo.
38
Walimwaga damu ya wasio na hatia, damu ya watoto wao wa kiume na wa kike ambao waliwatoa tambiko kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikatiwa unajisi kwa mauaji hayo.
39
Hivyo wakafanywa najisi kwa matendo yao, 2wakakosa uaminifu kwa Mungu kama wazinzi.
40
Hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawawakia watu wake, akachukizwa sana na hao waliokuwa mali yake.
41
Akawatia makuchani mwa watu wa mataifa, hao wenye kuwachukia wakawatawala.
42
Maadui zao waliwakandamiza, wakawatumikisha kwa nguvu.
43
Mara nyingi Mungu aliwaokoa watu wake, lakini wao wakachagua kumwasi, wakazidi kuzama katika uovu wao.
44
Hata hivyo Mungu alizijali taabu zao, wakati aliposikia kilio chao;
45
kwa ajili yao alilikumbuka agano lake, akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake.
46
Aliwafanya waliowakandamiza wawaonee huruma.
47
Utuokoe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, utukusanye pamoja kutoka kwa mataifa, tupate kulisifu jina lako takatifu, na kuona fahari juu ya sifa zako.
48
Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele! Na watu wote waseme: “Amina!” Asifiwe Mwenyezi-Mungu!
← Chapter 105
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 107 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150