bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Psalms 78
Psalms 78
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 77
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 79 →
1
(Utenzi wa Asafu) Sikieni mafundisho yangu, enyi watu wangu; yategeeni sikio maneno ya kinywa changu.
2
Nitasema nanyi kwa mafumbo, nitasema mambo yaliyofichika tangu kale;
3
mambo tuliyoyasikia na kuyajua, mambo ambayo wazee wetu walitusimulia.
4
Hatutawaficha watoto wetu; ila tutakisimulia kizazi kijacho matendo matukufu ya Mwenyezi-Mungu na uwezo wake; tutawaambia maajabu yake aliyotenda.
5
Aliwapa wazawa wa Yakobo masharti, aliweka sheria katika Israeli, ambayo aliwaamuru wazee wetu wawafundishe watoto wao;
6
ili watu wa kizazi kijacho, watoto watakaozaliwa baadaye, wazijue, nao pia wawajulishe watoto wao,
7
ili wamwekee Mungu tumaini lao, wasije wakasahau matendo ya Mungu, bali wazingatie amri zake.
8
Wasiwe kama walivyokuwa wazee wao, watu wakaidi na waasi; kizazi ambacho hakikuwa na msimamo thabiti, ambacho hakikuwa na uaminifu kwa Mungu.
9
Watu wa Efraimu, pinde na mishale mkononi, walirudi nyuma, wakakimbia siku ile ya vita.
10
Hawakulizingatia agano la Mungu; walikataa kufuata sheria yake.
11
Walisahau mambo aliyokuwa ametenda, miujiza aliyokuwa amewaonesha.
12
Alifanya maajabu mbele ya wazee wao, kondeni Soani, nchini Misri.
13
Aliigawa bahari, akawapitisha humo; aliyafanya maji yasimame kama ukuta.
14
Mchana aliwaongoza kwa wingu; usiku kucha kwa mwanga wa moto.
15
Aliipasua miamba kule jangwani, akawanywesha maji kutoka vilindini.
16
Alibubujisha vijito kutoka mwambani, akatiririsha maji kama mito.
17
Hata hivyo waliendelea kumkosea Mungu; walimwasi Mungu Mkuu kule jangwani.
18
Walimjaribu Mungu kwa makusudi; wakidai wapewe chakula walichotaka.
19
Walimkufuru Mungu wakisema: “Je, Mungu aweza kutupa chakula jangwani?
20
Ni kweli, aliupiga mwamba, maji yakabubujika kama mto; lakini, sasa aweza kweli kutupatia mkate, na kuwapatia watu wake nyama?”
21
Mwenyezi-Mungu, aliposikia hayo, alijawa na ghadhabu, moto ukawawakia wazawa wa Yakobo; hasira yake ikawavamia watu wa Israeli,
22
kwa sababu hawakuwa na imani naye, wala hawakuamini nguvu yake ya kuokoa.
23
Hata hivyo aliyaamuru mawingu ya juu, akaifungua milango ya mbingu;
24
akawanyeshea mana wale, akawapa nafaka kutoka mbinguni.
25
Binadamu, wakala chakula cha malaika; naye aliwapelekea chakula cha kutosha.
26
Alivumisha upepo wa mashariki, kwa nguvu yake akachochea pepo za kusini;
27
akawanyeshea watu wake nyama kama vumbi, ndege wengi kama mchanga wa pwani;
28
ndege hao walianguka kambini mwao, kila mahali kuzunguka makao yao.
29
Watu walikula wakashiba; Mungu aliwapa walichotaka.
30
Lakini hata kabla ya kutosheleza hamu yao, chakula kikiwa bado mdomoni mwao,
31
hasira ya Mungu iliwaka juu yao; akawaua wenye nguvu miongoni mwao, na kuwaangusha vijana wa Israeli.
32
Hata hivyo waliendelea kumkosea Mungu; ijapokuwa alitenda maajabu, hawakuamini.
33
Basi, akazikatisha siku zao kama pumzi, miaka yao kwa maafa ya ghafla.
34
Kila alipowaua, waliobaki walimgeukia; walitubu, wakamgeukia Mungu kwa moyo.
35
Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa mwamba wao; Mungu Mkuu alikuwa mkombozi wao.
36
Lakini walimdanganya kwa maneno yao; kila walichomwambia kilikuwa uongo.
37
Hawakuambatana naye kwa moyo, hawakuwa waaminifu kwa agano lake.
38
Lakini Mungu mwenye huruma alisamehe uovu wao, na wala hakuwaangamiza. Mara nyingi aliizuia hasira yake, wala hakuiacha ghadhabu yake yote iwake.
39
Alikumbuka kwamba wao ni watu tu; ni kama upepo upitao na kutoweka.
40
Mara ngapi walimwasi kule jangwani, na kumchukiza hukohuko nyikani!
41
Walimjaribu Mungu tena na tena, wakamkasirisha huyo Mtakatifu wa Israeli.
42
Hawakuikumbuka nguvu yake, wala siku ile alipowaokoa na maadui zao,
43
alipotenda maajabu nchini Misri, na miujiza kondeni Soani!
44
Aliigeuza ile mito kuwa damu, Wamisri wasipate maji ya kunywa.
45
Aliwapelekea makundi ya nzi waliowasumbua, na vyura waliowatia hasara.
46
Alituma nzige, wakala mavuno yao, na kuharibu mashamba yao.
47
Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe, na mitini yao kwa baridi kali.
48
Ngombe wao aliwaua kwa mvua ya mawe, na kondoo wao kwa radi.
49
Aliacha hasira yake kali iwawakie, ghadhabu, chuki na dhiki, na kundi la malaika waangamizi.
50
Aliachilia hasira yake iendelee, wala hakuwaepusha na kifo, bali aliwaangamiza kwa tauni.
51
Aliwaua wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri; naam, chipukizi wa kwanza kambini mwa Hamu.
52
Kisha aliwahamisha watu wake kama kondoo, akawaongoza jangwani kama kundi la mifugo.
53
Aliwaogoza salama, wala hawakuogopa; lakini bahari iliwafunika maadui zao.
54
Aliwaleta katika nchi yake takatifu, katika mlima aliouteka kwa nguvu yake.
55
Aliyafukuza mataifa mbele yao, akazitoa nchi zao ziwe mali ya Israeli, akayakalisha makabila ya Israeli mahemani mwao.
56
Hata hivyo walimjaribu na kumwasi Mungu Mkuu; wala hawakuzingatia masharti yake.
57
Ila waligeuka na kufanya mabaya kama wazee wao; wakayumbayumba kama upinde usio imara.
58
Walimkasirisha kwa madhabahu zao za miungu; wakamchochea aone wivu kwa sanamu zao za kuchonga.
59
Mungu alipoona hayo, akawaka hasira; akamkataa Israeli katakata.
60
Aliyaacha makao yake kule Shilo, makao ambamo alikaa kati ya watu.
61
Aliiacha ishara ya nguvu yake itekwe, utukufu wake utiwe mikononi mwa maadui.
62
Aliwakasirikia watu wake mwenyewe; akawatoa waangamizwe kwa upanga.
63
Moto ukawateketeza vijana wao wa kiume, na wasichana wao wakakosa wachumba.
64
Makuhani wao walikufa kwa upanga, wala wajane wao hawakuomboleza.
65
Kisha Bwana aliamka kama kutoka usingizini, kama shujaa aliyechangamshwa na divai.
66
Akawatimua maadui zake; akawatia aibu ya kudumu milele.
67
Lakini aliikataa jamaa ya Yosefu, wala hakulichagua kabila la Efraimu.
68
Ila alilichagua kabila la Yuda, mlima Siyoni anaoupenda.
69
Alijenga hapo hekalu lake kubwa kama mbingu, kama dunia aliyoiweka imara milele.
70
Alimchagua Daudi, mtumishi wake, akamtoa katika kazi ya kuchunga kondoo.
71
Alimtoa katika kazi ya kuchunga kondoo na wanakondoo, awe na jukumu la kuchunga watu wa Yakobo taifa lake. Achunge Israeli, watu wake Mungu mwenyewe.
72
Daudi akawafunza kwa moyo wake wote, akawaongoza kwa uhodari mkubwa.
← Chapter 77
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 79 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150