bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Psalms 119
Psalms 119
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 118
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 120 →
1
Heri watu wanaoishi bila kosa, wanaozingatia sheria ya Mwenyezi-Mungu.
2
Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote,
3
watu wasiotenda uovu kamwe, bali daima hufuata njia zake.
4
Ee Mungu, umetupatia kanuni zako ili tuzishike kwa uaminifu.
5
Laiti mwenendo wangu ungeimarika, kwa kuyafuata masharti yako!
6
Nikizingatia amri zako zote, hapo kweli sitaaibishwa.
7
Nitakusifu kwa moyo mnyofu, nikijifunza maagizo yako maadilifu.
8
Nitayafuata masharti yako; usiniache hata kidogo.
9
Kijana atatunzaje maisha yake kuwa safi? Kwa kuyaongoza kadiri ya neno lako.
10
Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako.
11
Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea.
12
Utukuzwe, ee Mwenyezi-Mungu! Unifundishe masharti yako.
13
Nitayarudia kwa sauti maagizo yako yote uliyotoa.
14
Nafurahi kufuata maamuzi yako, kuliko kuwa na utajiri mwingi.
15
Nazitafakari kanuni zako, na kuzizingatia njia zako.
16
Nayafurahia masharti yako; sitalisahau neno lako.
17
Unitendee mimi mtumishi wako kwa ukarimu, nipate kuishi na kushika neno lako.
18
Uyafumbue macho yangu, niyaone maajabu ya sheria yako.
19
Mimi ni mkimbizi tu hapa duniani; usinifiche amri zako.
20
Roho yangu yaugua kwa hamu kubwa ya kutaka kujua daima maagizo yako.
21
Wewe wawakemea wenye kiburi, walaanifu, ambao wanakiuka amri zako.
22
Uniepushe na matusi na madharau yao, maana nimeyazingatia maamuzi yako.
23
Hata kama wakuu wanakula njama dhidi yangu; mimi mtumishi wako nitayatafakari maamuzi yako.
24
Masharti yako ni furaha yangu; hayo ni washauri wangu.
25
Nagaagaa chini mavumbini; unipe tena uhai kama ulivyoahidi.
26
Nimeungama niliyotenda, nawe ukanijibu; unifundishe masharti yako.
27
Unifundishe namna ya kushika kanuni zako, nami nitayatafakari matendo yako ya ajabu.
28
Niko hoi kwa uchungu; unirudishie nguvu kama ulivyoahidi.
29
Uniepushe na njia za upotovu; unifundishe kwa wema sheria yako.
30
Nimechagua njia ya uaminifu; nimezingatia maagizo yako.
31
Nazingatia maamuzi yako, ee Mwenyezi-Mungu; usikubali niaibishwe!
32
Nitafuata maelekezo ya amri zako, maana unanipa maarifa zaidi.
33
Ee Mwenyezi-Mungu, unifundishe kutii masharti yako; nami nitayashika mpaka mwisho.
34
Unieleweshe nipate kuishika sheria yako, niifuate kwa moyo wangu wote.
35
Uniongoze katika njia ya amri zako, maana humo napata furaha yangu.
36
Unipe ari ya kuzingatia maamuzi yako, na si kwa ajili ya kupata faida isiyofaa.
37
Uniepushe, nisifuate mambo ya upuuzi; unioneshe njia yako, unipe uhai.
38
Unitimizie mimi mtumishi wako ahadi yako; ahadi unayowapa wale wanaokuheshimu.
39
Uniokoe na lawama ninazoogopa; maana maagizo yako ni mema.
40
Natamani sana kuzitii kanuni zako; unijalie uhai maana wewe ni mwadilifu.
41
Fadhili zako zinijie, ee Mwenyezi-Mungu; uniokoe kama ulivyoahidi.
42
Hapo nitaweza kuwajibu hao wanaonitukana, maana mimi nina imani sana na neno lako.
43
Unijalie kusema ukweli wako daima, maana tumaini langu liko katika maagizo yako.
44
Nitatii sheria yako daima, nitaishika milele na milele.
45
Nitaishi katika uhuru kamili, maana nazitilia maanani kanuni zako.
46
Nitawatangazia wafalme maamuzi yako, wala sitaona aibu.
47
Furaha yangu ni kuzitii amri zako, ambazo mimi nazipenda.
48
Naziheshimu na kuzipenda amri zako; nitayatafakari masharti yako.
49
Ukumbuke ahadi yako kwangu mimi mtumishi wako, ahadi ambayo imenipa matumaini.
50
Hata niwapo taabuni napata kitulizo, maana ahadi yako yanipa uhai.
51
Wasiomjali Mungu hunidharau daima, lakini mimi sikiuki sheria yako.
52
Ninapoyakumbuka maagizo yako ya tangu kale, nafarijika, ee Mwenyezi-Mungu.
53
Nashikwa na hasira kali, nionapo waovu wakivunja sheria yako.
54
Masharti yako yamekuwa wimbo wangu, nikiwa huku ugenini.
55
Usiku ninakukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, na kushika sheria yako.
56
Hii ni baraka kubwa kwangu, kwamba nazishika kanuni zako.
57
Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe riziki yangu kuu; naahidi kushika maneno yako.
58
Naomba radhi yako kwa moyo wangu wote; unionee huruma kama ulivyoahidi!
59
Nimeufikiria mwenendo wangu, na nimerudi nifuate maamuzi yako.
60
Bila kukawia nafanya haraka kuzishika amri zako.
61
Waovu wametega mitego waninase, lakini mimi sisahau sheria yako.
62
Usiku wa manane naamka kukusifu, kwa sababu ya maagizo yako maadilifu.
63
Mimi ni rafiki ya wote wakuchao, rafiki yao wanaozitii kanuni zako.
64
Dunia imejaa fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, unifundishe masharti yako.
65
Umenitendea vema mimi mtumishi wako, kama ulivyoahidi, ee Mwenyezi-Mungu.
66
Unifundishe akili na maarifa, maana nina imani sana na amri zako.
67
Kabla ya kuniadhibu nilikuwa nikikosea, lakini sasa nashika neno lako.
68
Wewe ni mwema na mfadhili; unifundishe masharti yako.
69
Wenye kiburi wanasema uongo juu yangu, lakini mimi nashika kanuni zako kwa moyo wote.
70
Mioyo yao imejaa upumbavu, lakini mimi nafurahia sheria yako.
71
Nimefaidika kutokana na taabu yangu, maana imenifanya nijifunze masharti yako.
72
Sheria uliyoweka ni bora kwangu, kuliko mali zote za dunia.
73
Mikono yako iliniumba na kuniunda; unijalie akili nijifunze amri zako.
74
Wakuchao wataniona na kufurahi, maana tumaini langu liko katika neno lako.
75
Najua hukumu zako ni adili, ee Mwenyezi-Mungu, na kwamba umeniadhibu kwani wewe ni mwaminifu.
76
Fadhili zako na zinipe faraja, kama ulivyoniahidi mimi mtumishi wako.
77
Unionee huruma nipate kuishi, maana sheria yako ni furaha yangu.
78
Wenye kiburi waaibike kwa maana wamenifanyia hila, lakini mimi nitazitafakari kanuni zako.
79
Wote wakuchao na waje kwangu, wapate kuyajua maamuzi yako.
80
Moyo wangu na uzingatie masharti yako, nisije nikaaibishwa.
81
Niko hoi kwa kukungojea uniokoe; naweka tumaini langu katika neno lako.
82
Macho yangu yanafifia nikingojea ulichoahidi. Nauliza: “Utakuja lini kunifariji?”
83
Nimekunjamana kama kiriba katika moshi, hata hivyo sijasahau masharti yako.
84
Mimi mtumishi wako nitasubiri mpaka lini? Utawaadhibu lini wale wanaonidhulumu?
85
Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, watu ambao hawafuati sheria yako.
86
Amri zako zote ni za kuaminika; watu wananitesa bila haki; unisaidie!
87
Karibu wangefaulu kuniangamiza, lakini mimi sijavunja kanuni zako.
88
Unisalimishe kadiri ya fadhili zako, nipate kuzingatia maamuzi uliyotamka.
89
Neno lako, ee Mwenyezi-Mungu, ladumu milele; limethibitika juu mbinguni.
90
Uaminifu wako wadumu vizazi vyote, umeiweka dunia mahali pake nayo yadumu.
91
Kwa amri yako viumbe vyote vipo leo, maana vitu vyote ni watumishi wako.
92
Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningalikwisha angamia kwa taabu zangu.
93
Sitasahau kamwe kanuni zako, maana kwa hizo umenipa uhai.
94
Mimi ni wako, uniokoe, maana nimejitahidi kuzishika kanuni zako.
95
Waovu wanivizia wapate kuniua; lakini mimi natafakari masharti yako.
96
Nimetambua kila kitu hufikia kikomo, lakini amri yako ni kamilifu.
97
Naipenda sana sheria yako! Naitafakari mchana kutwa!
98
Amri yako iko nami daima, yanipa hekima kuliko maadui zangu.
99
Ninaelewa kuliko waalimu wangu wote, kwa kuwa nayatafakari maamuzi yako.
100
Nawapita wazee kwa busara yangu, kwa sababu nazishika kanuni zako.
101
Najizuia nisifuate njia mbaya, nipate kulizingatia neno lako.
102
Sikukiuka maagizo yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha.
103
Maneno yako ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali!
104
Kwa kanuni zako napata hekima, kwa hiyo nachukia kila mwenendo mbaya.
105
Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.
106
Nimeapa na kuthibitisha kiapo changu, kwamba nitashika maagizo yako adili.
107
Ee Mwenyezi-Mungu, ninateseka mno; unijalie uhai kama ulivyoahidi.
108
Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako.
109
Maisha yangu yamo hatarini daima, lakini siisahau sheria yako.
110
Waovu wamenitegea mitego, lakini sikiuki kanuni zako.
111
Maamuzi yako ni riziki kubwa kwangu milele; hayo ni furaha ya moyo wangu.
112
Nimekusudia kwa moyo wote kufuata masharti yako milele.
113
Nawachukia watu wanafiki, lakini naipenda sheria yako.
114
Wewe ni ngao yangu, kwako napata usalama; naweka tumaini langu katika neno lako.
115
Ondokeni kwangu, enyi waovu, ili nipate kushika amri za Mungu wangu.
116
Uniimarishe ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali niaibike katika tumaini langu.
117
Unitegemeze, niwe salama; niwe daima msikivu kwa masharti yako.
118
Unawakataa wote wanaokiuka masharti yako; mawazo yao maovu ni ya bure.
119
Waovu wote wawaona kuwa takataka, kwa hiyo mimi napenda maamuzi yako.
120
Natetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya hukumu zako.
121
Nimefanya mambo mema na adili; usiniache makuchani mwa maadui zangu.
122
Uahidi kunisaidia mimi mtumishi wako; usikubali wenye kiburi wanidhulumu.
123
Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi.
124
Unitendee mimi mtumishi wako kadiri ya wema wako, unifundishe masharti yako.
125
Mimi ni mtumishi wako, unipe maarifa, nipate kujua maamuzi yako.
126
Ee Mwenyezi-Mungu, sasa ni wakati wa kufanya kitu, kwa maana watu wanavunja sheria yako.
127
Mimi, nazipenda amri zako, kuliko hata dhahabu safi kabisa.
128
Kwa hiyo, nafuata kanuni zako zote; kila njia potovu naichukia.
129
Maamuzi yako ni ya ajabu; kwa hiyo nayashika kwa moyo wote.
130
Maelezo ya mafundisho yako huleta mwanga; huwapa akili watu wasiojua kitu.
131
Nafungua kinywa kwa hamu kubwa, maana ninatamani sana amri zako.
132
Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda.
133
Uniimarishie hatua zangu kama ulivyoahidi; usikubali mimi nitawaliwe na uovu.
134
Unikomboe kutoka udhalimu wa binadamu, ili nipate kuzishika kanuni zako.
135
Uniangazie uso wako kwa wema, unifundishe masharti yako.
136
Macho yangu yabubujika machozi kama mto, kwa sababu watu hawaishiki sheria yako.
137
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu; na hukumu zako ni za haki.
138
Umetoa maamuzi yako, kwa haki na uthabiti.
139
Upendo wangu kwako wanifanya niwake hasira, maana maadui zangu hawajali maneno yako.
140
Ahadi yako ni hakika kabisa, nami mtumishi wako naipenda.
141
Mimi ni mdogo na ninadharauliwa; hata hivyo sisahau kanuni zako.
142
Uadilifu wako ni wa haki milele; sheria yako ni ya kweli.
143
Taabu na huzuni vimenipata, lakini amri zako ndizo furaha yangu.
144
Maamuzi yako ni ya haki daima; unijalie maarifa nipate kuishi.
145
Nakulilia kwa moyo wangu wote; unijibu, ee Mwenyezi-Mungu, nifuate kanuni zako.
146
Nakulilia, unisalimishe; nipate kuyazingatia maamuzi yako.
147
Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako.
148
Nakaa macho usiku kucha, ili nitafakari juu ya maagizo yako.
149
Kwa fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, unisikie; unisalimishe kwa uadilifu wako.
150
Wale wanaonidhulumu vibaya wanakaribia, hao wako mbali kabisa na sheria yako.
151
Lakini wewe u karibu nami, ee Mwenyezi-Mungu, na amri zako zote ni za kuaminika.
152
Tangu zamani, nimejifunza maamuzi yako; ambayo umeyaweka hata yadumu milele.
153
Uangalie mateso yangu, uniokoe, kwa maana sikuisahau sheria yako.
154
Unitetee na kunikomboa; unijalie uhai kama ulivyoahidi.
155
Waovu hawataokolewa kamwe, maana hawajali juu ya masharti yako.
156
Huruma yako ni kubwa, ee Mwenyezi-Mungu, unijalie uhai kama ulivyoahidi.
157
Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako.
158
Niwaonapo wahaini hao nachukizwa mno, kwa sababu hawazishiki amri zako.
159
Tazama, ee Mungu, ninavyozipenda kanuni zako! Unijalie uhai kadiri ya fadhili zako.
160
Kitovu cha neno lako ni ukweli, maagizo yako yote adili, yadumu milele.
161
Wakuu wanidhulumu bila kisa, lakini mimi naheshimu maneno yako kwa moyo wote.
162
Nafurahi kwa sababu ya neno lako, kama mtu aliyekuta kitu cha thamani kuu.
163
Nachukia kabisa uongo, lakini naipenda sheria yako.
164
Nakusifu mara saba kila siku, kwa sababu ya maagizo yako adili.
165
Wapendao sheria yako wana amani kuu; hakuna kinachoweza kuwaangusha.
166
Ee Mwenyezi-Mungu, nakungojea uniokoe; mimi natimiza amri zako.
167
Nazingatia maamuzi yako; nayapenda kwa moyo wote.
168
Nazingatia kanuni na maamuzi yako; wewe wauona mwenendo wangu wote.
169
Kilio changu kikufikie, ee Mwenyezi-Mungu! Unijalie akili kama ulivyoahidi.
170
Ombi langu likufikie; uniokoe kama ulivyoahidi.
171
Nitasema sifa zako mfululizo, maana wanifundisha masharti yako.
172
Nitaimba juu ya neno lako, maana amri zako zote ni za haki.
173
Uwe daima tayari kunisaidia, maana nimeamua kufuata kanuni zako.
174
Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu.
175
Unijalie kuishi nipate kukusifu; na maagizo yako yanisaidie.
176
Natangatanga kama kondoo aliyepotea; uje kunitafuta mimi mtumishi wako, maana sikusahau amri zako.
← Chapter 118
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 120 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150