bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Ezekiel 7
Ezekiel 7
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 8 →
1
Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema:
2
“Mwanadamu, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa nchi ya Israeli: “ ‘Mwisho! Mwisho umekuja juu ya pembe nne za nchi!
3
Sasa mwisho umekuja juu yenu, nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza.
4
Sitawaonea huruma wala kuwarehemu. Hakika nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’
5
“Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “ ‘Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa! Tazama, yanakuja!
6
Mwisho umewadia! Mwisho umewadia! Umejiinua wenyewe dhidi yenu. Tazama, umewadia!
7
Maangamizi yamekuja juu yenu, ninyi mnaoishi katika nchi. Wakati umewadia! Siku imekaribia! Kuna hofu kuu ya ghafula juu ya milima, wala si furaha.
8
Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenu na kumaliza hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo.
9
Sitawaonea huruma wala kuwarehemu. Nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi za machukizo miongoni mwenu. “ ‘Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu ambaye huwapiga.
10
“ ‘Tazama, siku imefika! Tazama, imewadia! Maangamizi yamezuka ghafula, fimbo imechanua, nayo majivuno yamechipua!
11
Jeuri imeinuka kuwa fimbo ya kuadhibu waovu. Hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa, hata mmoja wa kundi hilo: hakuna utajiri wao utabaki, wala chochote cha thamani.
12
Wakati umewadia, siku imefika. Mnunuzi na asifurahi wala muuzaji asihuzunike, kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote.
13
Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai. Kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake.
14
“ ‘Wajapopiga tarumbeta na kuweka kila kitu tayari, hakuna hata mmoja atakayeenda vitani, kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote.
15
Nje ni upanga, ndani ni tauni na njaa. Walio shambani watakufa kwa upanga, nao waliomo mjini njaa na tauni vitawala.
16
Wote watakaopona na kutoroka watakuwa milimani, wakiomboleza kama hua wa mabondeni, kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake.
17
Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji.
18
Watavaa gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu, na vichwa vyao vitanyolewa.
19
“ ‘Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Hawatashibisha njaa yao au kujaza tumbo zao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini.
20
Walijivunia vito vyao vizuri na kuvitumia kutengeneza sanamu za machukizo na vinyago vya upotovu. Kwa hiyo nitavifanya vitu hivyo kuwa najisi kwao.
21
Nitavitia vyote mikononi mwa wageni kuwa nyara na kuwa vitu vilivyotekwa mikononi mwa watu waovu wa dunia, nao watavinajisi.
22
Nitaugeuza uso wangu mbali nao, nao waovu wa dunia watapanajisi mahali pangu pa thamani. Wanyang’anyi watapaingia na kupanajisi.
23
“ ‘Andaa minyororo, kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damu na mji umejaa udhalimu.
24
Nitaleta taifa ovu kuliko yote kumiliki nyumba zao. Nitakomesha kiburi cha wenye nguvu na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi.
25
Hofu ya ghafula itakapokuja, watatafuta amani, lakini haitapatikana.
26
Maafa juu ya maafa yatakuja, tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya. Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii; mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea, vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee.
27
Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawaadhibu kulingana na matendo yao, na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. “ ‘Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ”
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48