bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Ezekiel 8
Ezekiel 8
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 9 →
1
Katika mwaka wa sita, siku ya tano ya mwezi wa sita, nilipokuwa nimeketi katika nyumba yangu na wazee wa Yuda wakiwa wameketi mbele yangu, mkono wa Bwana Mungu Mwenyezi ulikuja juu yangu.
2
Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kiuno kuelekea juu sura yake iling’aa vile chuma king’aavyo kikiwa ndani ya moto.
3
Akanyoosha kitu kilichofanana na mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho wa Mungu akaniinua juu kati ya nchi na mbingu, na nikiwa katika maono ya Mungu, akanichukua hadi Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la kaskazini mwa ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu inayochochea wivu.
4
Tazama! Palikuwa na utukufu wa Mungu wa Israeli, kama utukufu ule niliouona katika maono kule kwenye nchi tambarare.
5
Kisha akaniambia, “Mwanadamu, tazama kuelekea kaskazini.” Hivyo nikatazama na kwenye ingilio la kaskazini mwa lango la madhabahu, nikaona sanamu hii ya wivu.
6
Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayoyafanya: mambo ya kuchukiza kabisa ambayo nyumba ya Israeli wanayatenda hapa, yatakayonifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utayaona mambo yanayochukiza hata zaidi.”
7
Kisha akanileta hadi ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani.
8
Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango.
9
Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.”
10
Hivyo nikaingia ndani na kutazama. Nikaona kuta zote zimechorwa aina mbalimbali ya viumbe vinavyotambaa, na wanyama wanaochukiza, na sanamu zote za nyumba ya Israeli.
11
Mbele ya hizo kuta walisimama wazee sabini wa nyumba ya Israeli, naye Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama miongoni mwao. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi, na moshi wa harufu nzuri ya uvumba ulikuwa unapanda juu.
12
Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa Israeli wakiwa gizani, kila mmoja kwenye mahali pa ibada pa sanamu yake? Wao husema, ‘Mwenyezi Mungu hatuoni, Mwenyezi Mungu ameiacha nchi.’ ”
13
Akasema tena, “Utawaona wakifanya mambo yaliyo chukizo zaidi.”
14
Ndipo akanileta kwenye ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi Mungu, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi.
15
Akaniambia, “Je, mwanadamu, unaliona hili? Utayaona mambo yanayochukiza hata zaidi.”
16
Ndipo akanileta hadi kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, na katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, palikuwa na wanaume wapatao ishirini na watano. Walikuwa wamelipa kisogo Hekalu la Mwenyezi Mungu na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua upande wa mashariki.
17
Akaniambia, “Je, umeona hili mwanadamu? Je, ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda kufanya machukizo wanayoyafanya hapa? Je, ni lazima pia waijaze nchi dhuluma na kuendelea siku zote kunikasirisha? Watazame wanavyonibania pua kana kwamba ninanuka!
18
Kwa hiyo nitawaadhibu kwa hasira; sitawaonea huruma wala kuwarehemu. Hata wakipiga makelele masikioni mwangu, sitawasikiliza.”
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48