bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Genesis 14
Genesis 14
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 15 →
1
Wakati huo Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu
2
walienda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari).
3
Wafalme wa kundi hili la pili waliunganisha majeshi yao katika Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi).
4
Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na mbili, lakini mwaka wa kumi na tatu wakaasi.
5
Mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walienda vitani na wakawashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,
6
na Wahori katika nchi ya vilima ya Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa.
7
Kisha wakarudi, wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori walioishi Hasason-Tamari.
8
Ndipo mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu
9
dhidi ya Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari; yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano.
10
Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani.
11
Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao.
12
Pia walimteka Lutu, mwana wa ndugu yake Abramu, pamoja na mali yake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma.
13
Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, ndugu ya Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu.
14
Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu mia tatu na kumi na nane (318) wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani.
15
Wakati wa usiku, Abramu aliwapanga watu wake katika vikosi, wakawashambulia na kuwashinda, wakawafukuza hadi Hoba, kaskazini mwa Dameski.
16
Abramu akarudisha mali yote, na akamrudisha Lutu jamaa yake na mali yake, pamoja na wanawake na watu wengine.
17
Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme).
18
Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.
19
Naye akambariki Abramu, akisema, “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na nchi.
20
Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana, ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.” Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.
21
Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu, nawe uchukue hizo mali.”
22
Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa
23
kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’
24
Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula, na sehemu ambayo ni fungu la watu walioenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.”
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50