bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Genesis 2
Genesis 2
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 3 →
1
Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.
2
Kufikia siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya; hivyo siku hiyo ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote.
3
Mungu akaibariki siku ya saba, akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika baada ya kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.
4
Haya ndio maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. Bwana Mwenyezi Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
5
hapakuwa na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwa na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kuilima ardhi,
6
lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi.
7
Bwana Mwenyezi Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.
8
Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni; huko akamweka huyo mtu aliyemuumba.
9
Bwana Mwenyezi Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Mti wa uzima ulikuwa katikati ya bustani, na pia mti wa kujua mema na mabaya.
10
Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni; kuanzia hapo ukagawanyika kuwa mito minne.
11
Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu.
12
(Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri; bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.)
13
Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi.
14
Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.
15
Bwana Mwenyezi Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza.
16
Bwana Mwenyezi Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani;
17
lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”
18
Bwana Mwenyezi Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”
19
Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ametengeneza kutoka ardhi wanyama pori wote, na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa jina lake.
20
Hivyo Adamu akawapa majina mifugo wote, ndege wa angani, na wanyama pori wote. Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.
21
Hivyo Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama.
22
Kisha Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwa ule ubavu alioutoa kwa mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa mwanaume.
23
Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke’, kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”
24
Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25
Adamu na mkewe wote walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50