bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Genesis 49
Genesis 49
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 50 →
1
Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni, mnizunguke ili niweze kuwaambia yale yatakayowatokea siku zijazo.
2
“Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo; msikilizeni baba yenu Israeli.
3
“Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu; umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo.
4
Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi.
5
“Simeoni na Lawi ni ndugu: panga zao ni silaha za jeuri.
6
Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, na kukata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.
7
Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! Nitawatawanya katika Yakobo, na kuwasambaza katika Israeli.
8
“Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; wana wa baba yako watakusujudia.
9
Ee Yuda, wewe ni mwana simba; unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba hunyemelea na kulala chini, kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha?
10
Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake.
11
Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu.
12
Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
13
“Zabuloni ataishi pwani ya bahari na kuwa bandari za kuegesha meli; mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni.
14
“Isakari ni punda mwenye nguvu ambaye amelala kati ya mizigo yake.
15
Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika na jinsi nchi yake inavyopendeza, atainamisha bega lake kwenye mzigo na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu.
16
“Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli.
17
Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali.
18
“Ee Mwenyezi Mungu, nautafuta wokovu wako.
19
“Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa.
20
“Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kinachomfaa mfalme.
21
“Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri.
22
“Yusufu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani.
23
Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili.
24
Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,
25
kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za juu mbinguni, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
26
Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
27
“Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”
28
Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka iliyomfaa.
29
Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
30
pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua liwe mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
31
Huko ndiko Ibrahimu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaka na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea.
32
Shamba hilo na pango lililo ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”
33
Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 50 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50