bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Genesis 17
Genesis 17
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 18 →
1
Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi Mungu akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; nenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.
2
Nitafanya agano kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana.”
3
Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia,
4
“Kwangu mimi, hili ndilo agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi.
5
Hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Ibrahimu, kwa maana nimekufanya baba wa mataifa mengi.
6
Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana; kwako yatatoka mataifa, na wafalme watatoka kwako.
7
Nitalithibitisha agano langu kama agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo, nami nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
8
Nchi yote ya Kanaani, unayoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na ya uzao wako; nami nitakuwa Mungu wao.”
9
Ndipo Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwako wewe, lazima ushike agano langu, wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo.
10
Hili ni agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa.
11
Mtatahiriwa, na hii itakuwa ni alama ya agano kati yangu na ninyi.
12
Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio wa uzao wako.
13
Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima atahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni agano la milele.
14
Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.”
15
Pia Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai, bali jina lake litakuwa Sara.
16
Nitambariki, na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki ili awe mama wa mataifa; wafalme wa mataifa watatoka kwake.”
17
Ibrahimu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?”
18
Ibrahimu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”
19
Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaka. Nitalithibitisha agano langu naye kama agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.
20
Kuhusu Ishmaeli, nimekusikia. Hakika nitambariki; nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.
21
Lakini agano langu nitalithibitisha kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.”
22
Alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, Mungu akaondoka kwa Ibrahimu.
23
Siku hiyo hiyo, Ibrahimu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake, pamoja na wale walionunuliwa kwa fedha zake; kila mwanaume wa nyumbani mwake akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza.
24
Ibrahimu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa;
25
naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na tatu.
26
Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku hiyo hiyo.
27
Wanaume wote nyumbani mwa Ibrahimu, waliozaliwa nyumbani mwake na walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa wageni, walitahiriwa pamoja naye.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50