bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Genesis 36
Genesis 36
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 37 →
1
Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).
2
Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti Eloni Mhiti, Oholibama binti Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi;
3
pia akaoa Basemathi binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
4
Ada akamzalia Esau Elifazi; Basemathi akamzaa Reueli;
5
Oholibama akawazaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.
6
Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, na watu wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote, na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.
7
Mali yao ilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja; nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
8
Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya vilima ya Seiri.
9
Hivi ndivyo vizazi vya Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya vilima ya Seiri.
10
Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
11
Wana wa Elifazi ni: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.
12
Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, aliyemzalia Amaleki. Hao walikuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.
13
Wana wa Reueli ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hao walikuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.
14
Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni: Yeushi, Yalamu na Kora.
15
Hawa walikuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: Temani, Omari, Sefo, Kenazi,
16
Kora, Gatamu na Amaleki. Hao walikuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu; walikuwa wajukuu wa kiume wa Ada.
17
Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu; walikuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.
18
Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni: Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.
19
Hao walikuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hao walikuwa wakuu wao.
20
Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, walioishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
21
Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.
22
Wana wa Lotani walikuwa: Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
23
Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
24
Wana wa Sibeoni walikuwa: Aya na Ana. (Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda wa Sibeoni, baba yake.)
25
Watoto wa Ana walikuwa: Dishoni na Oholibama binti Ana.
26
Wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
27
Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani.
28
Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani.
29
Hawa walikuwa wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
30
Dishoni, Eseri na Dishani. Hao walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.
31
Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:
32
Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
33
Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
34
Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
35
Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
36
Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
37
Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ng’ambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.
38
Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
39
Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
40
Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao: Timna, Alva, Yethethi,
41
Oholibama, Ela, Pinoni,
42
Kenazi, Temani, Mibsari,
43
Magdieli na Iramu. Hao walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki. Hivi ndivyo vizazi vya Esau, baba wa Waedomu.
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 37 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50