bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Proverbs 17
Proverbs 17
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
1
Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.
2
Mtumishi mwenye hekima atamtawala mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.
3
Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali Mwenyezi Mungu huujaribu moyo.
4
Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.
5
Yeye anaye mdhihaki maskini huonesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.
6
Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
7
Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!
8
Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa.
9
Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, bali yeyote arudiaye jambo huwatenganisha rafiki wa karibu.
10
Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
11
Mwovu hupenda kuasi tu; mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.
12
Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.
13
Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.
14
Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.
15
Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Mwenyezi Mungu huwachukia sana wote wawili.
16
Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, wakati yeye hana haja ya kupata hekima?
17
Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.
18
Mtu mjinga huutoa mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake.
19
Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu.
20
Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
21
Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.
22
Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
23
Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri ili kupotosha njia ya haki.
24
Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia.
25
Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa.
26
Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.
27
Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.
28
Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima akinyamaza, na mwenye ufahamu akiuzuia ulimi wake.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31