bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Proverbs 18
Proverbs 18
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 19 →
1
Mtu ajitengaye na wengine hufuata matakwa yake mwenyewe; hupiga vita kila shauri jema.
2
Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe.
3
Uovu unapokuja, dharau huja pia; pamoja na aibu huja lawama.
4
Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.
5
Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, au kumnyima haki asiye na hatia.
6
Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo.
7
Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.
8
Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu.
9
Mtu aliye mlegevu katika kazi yake ni ndugu na yule anayeharibu.
10
Jina la Mwenyezi Mungu ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama.
11
Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.
12
Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.
13
Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza, huo ni upumbavu wake na aibu yake.
14
Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?
15
Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
16
Zawadi humfungulia njia mtoaji, nayo humleta mbele ya wakuu.
17
Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi, hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.
18
Kupiga kura hukomesha mashindano na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
19
Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika kuliko mji uliozungushiwa ngome, nayo mabishano ni kama malango ya ngome yenye makomeo.
20
Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake, atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
21
Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao wanaoupenda watakula matunda yake.
22
Mtu anayepata mke anapata kitu chema, naye anajipatia kibali kwa Mwenyezi Mungu.
23
Mtu maskini huomba kuhurumiwa bali tajiri hujibu kwa ukali.
24
Mtu aliye na rafiki wasioaminika huangamia upesi, bali yuko rafiki anayeambatana na mtu kwa karibu kuliko ndugu.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31