bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Proverbs 5
Proverbs 5
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 6 →
1
Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
2
ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa.
3
Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4
lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili.
5
Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.
6
Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.
7
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.
8
Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
9
usije ukapoteza heshima yako kwa wengine, na miaka yako kwa aliye mkatili,
10
wageni wasije wakasherehekea utajiri wako, na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.
11
Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12
Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
13
Sikuwatii walimu wangu, wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
14
Nimefika ukingoni mwa maangamizi katika kusanyiko la watu wa Mungu.”
15
Kunywa maji kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kisima chako mwenyewe.
16
Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?
17
Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.
18
Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
19
Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.
20
Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?
21
Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Mwenyezi Mungu, naye huyapima mapito yake yote.
22
Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.
23
Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31