bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Proverbs 7
Proverbs 7
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
1
Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako.
2
Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3
Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako.
4
Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako;
5
watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza.
6
Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha.
7
Niliona miongoni mwa wajinga, nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, kijana asiye na akili.
8
Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9
wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia.
10
Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya hila.
11
(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;
12
mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)
13
Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:
14
“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.
15
Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!
16
Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17
Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.
18
Njoo, tuzame katika mapenzi hadi asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19
Mume wangu hayupo nyumbani; ameenda safari ya mbali.
20
Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwa nyumbani karibuni.”
21
Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.
22
Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23
hadi mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.
24
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.
25
Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.
26
Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.
27
Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31