bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Psalms 78
Psalms 78
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 77
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 79 →
1
Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu.
2
Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:
3
yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia.
4
Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Mwenyezi Mungu, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.
5
Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao,
6
ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.
7
Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao hawangesahau matendo yake, bali wangezishika amri zake.
8
Hawangefanana na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwa Mungu, ambao roho zao hazikumwamini.
9
Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita.
10
Hawakulishika agano la Mungu, na walikataa kuishi kwa sheria yake.
11
Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonesha.
12
Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri.
13
Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta.
14
Aliwaongoza kwa wingu mchana, na kwa nuru ya moto usiku kucha.
15
Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari,
16
alitoa vijito kutoka jabali lililochongoka, akayafanya maji yatiririke kama mito.
17
Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.
18
Kwa makusudi walimjaribu Mungu, wakidai vyakula walivyovitamani.
19
Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?
20
Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, vijito vikatiririka maji mengi. Lakini je, aweza kutupatia chakula pia? Je, anaweza kuwapatia watu wake nyama?”
21
Mwenyezi Mungu alipowasikia, alikasirika sana, moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli,
22
kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake.
23
Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu,
24
akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni.
25
Watu walikula mkate wa malaika, akawatumia chakula chote ambacho wangeweza kula.
26
Aliachia upepo wa mashariki kutoka mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake.
27
Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, ndege warukao kama mchanga wa pwani.
28
Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, kuzunguka mahema yao yote.
29
Walikula na kusaza, kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.
30
Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,
31
hasira ya Mungu ikawaka juu yao, akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, akiwaangusha vijana wa Israeli.
32
Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini.
33
Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho.
34
Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku.
35
Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.
36
Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao,
37
mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
38
Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote.
39
Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.
40
Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani!
41
Walimjaribu Mungu mara kwa mara, wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
42
Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,
43
siku aliyoonesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani.
44
Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.
45
Aliwapelekea makundi ya inzi wakawala, na vyura wakawaharibu.
46
Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige.
47
Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.
48
Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.
49
Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu.
50
Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni.
51
Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.
52
Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.
53
Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao.
54
Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.
55
Aliyafukuza mataifa mbele yao, na kuwagawia nchi zao kama urithi, aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.
56
Lakini wao walimjaribu Mungu, na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, wala hawakuzishika sheria zake.
57
Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, wakawa wasioweza kutegemewa kama upinde wenye kasoro.
58
Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.
59
Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa.
60
Akaiacha maskani ya Shilo, hema alilokuwa ameliweka katikati ya wanadamu.
61
Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui.
62
Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake.
63
Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,
64
makuhani wao waliuawa kwa upanga, wala wajane wao hawakuweza kulia.
65
Ndipo Bwana alipoamka kama kuamka usingizini, kama shujaa anavyoamka kutoka bumbuazi la mvinyo.
66
Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele.
67
Ndipo alipoyakataa mahema ya Yusufu, hakulichagua kabila la Efraimu,
68
lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda.
69
Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele.
70
Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.
71
Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake.
72
Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.
← Chapter 77
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 79 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150