bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Jeremiah 1
Jeremiah 1
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 2 →
1
Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi katika nchi ya Benyamini.
2
Neno la BWANA lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,
3
pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa kutawala kwake Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa kwenda uhamishoni.
4
Neno la BWANA lilinijia, kusema,
5
“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua; kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum; nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”
6
Nami nikasema, “Aa, BWANA Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”
7
Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utakwenda po pote nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza.
8
Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema BWANA.
9
Kisha BWANA akaunyosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.
10
Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung'oa na kubomoa, ili kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda.”
11
Neno la BWANA likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?” Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.”
12
BWANA akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”
13
Neno la BWANA likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka kikiwa kimeinama mdomo wake kuelekea upande wa kaskazini.”
14
BWANA akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi.
15
Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema BWANA. “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka na dhidi ya miji yote ya Yuda.
16
Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.
17
“Jiandae! Simama nawe useme cho chote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao.
18
Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.
19
Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe nami nitakuokoa,” asema BWANA.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52