bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Jeremiah 40
Jeremiah 40
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 41 →
1
Neno likamjia Yeremia kutoka kwa BWANA baada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa kifalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli.
2
Kiongozi wa walinzi alipomwona Yeremia, akamwambia, “BWANA Mungu wako aliamuru maafa haya kwa ajili ya mahali hapa.
3
Sasa BWANA ameyaleta haya, amefanya sawasawa na alivyosema kwamba angefanya. Yote haya yametokea kwa sababu ninyi watu mlifanya dhambi dhidi ya BWANA na hamkumtii.
4
Lakini leo ninakufungua kutoka minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Twende pamoja mpaka Babeli ikiwa unataka, nami nitakutunza, lakini kama hutaki basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda ko kote unakotaka.”
5
Hata hivyo kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au nenda po pote panapokupendeza.” Kisha huyo kiongozi akampa mahitaji yake na zawadi na akamwacha aende zake.
6
Kwa hiyo Yeremia akaenda kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mizpa na kuishi naye miongoni mwa watu walioachwa katika nchi.
7
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi naye amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini sana katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli,
8
wakamjia Gedalia huko Mizpa, ambao ni Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani na Yonathani wana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi, wana wa Efai Mnetofa na Yezania mwana wa Mmaaka pamoja na watu wao.
9
Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani akaapa kuwahakikishia tena wao na watu wao akisema: “Msiogope kuwatumikia Wakaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, nayo yote yatakuwa mema kwenu.
10
Mimi mwenyewe nitakaa Mizpa ili kuwawakilisha ninyi mbele ya Wakaldayo wanaotujia, lakini ninyi mtavuna divai, matunda ya kiangazi na mafuta, nanyi mtaweka katika vyombo vyenu vya kuhifadhia na kuishi katika miji mliyojitwalia.”
11
Wayahudi wote walioko Moabu, Amoni, Edomu na nchi nyingine zote waliposikia kwamba mfalme wa Babeli ameacha mabaki ya watu katika Yuda na amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kuwa mtawala wao,
12
wakarudi wote katika nchi ya Yuda kwa Gedalia huko Mizpa, kutoka nchi zote ambazo walikuwa wametawanywa. Nao wakavuna divai na matunda tele wakati wa kiangazi.
13
Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi wakamjia Gedalia huko Mizpa
14
na kumwambia, “Je, hujui kwamba Baalisi mfalme wa Waamoni amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania akuue?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu hakuwaamini.
15
Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko katika Mizpa. “Acha niende nikamwue Ishmaeli mwana wa Nethania wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokusanyika kukuzunguka watawanyike na mabaki wa Yuda waangamie?”
16
Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu akamwambia Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo kama hilo! Unalosema kuhusu Ishmaeli si kweli.”
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 41 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52