bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Jeremiah 10
Jeremiah 10
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 11 →
1
Sikieni lile ambalo BWANA, anena nanyi Ee nyumba ya Israeli.
2
Hili ndilo asemalo BWANA: “Usijifunze njia za mataifa wala usitishwe na ishara katika anga, ingawa mataifa yanatishwa nazo.
3
Kwa maana desturi za mataifa hazina maana, wanakata mti kutoka msituni na fundi anauchonga kwa patasi.
4
Wanaparemba kwa fedha na dhahabu, wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike.
5
Sanamu zao ni kama sanamu iliyowekwa shambani kutishia ndege kwenye shamba la matango, nazo haziwezi kuongea; sharti zibebwe kwa sababu haziwezi kutembea. Usiziogope; haziwezi kudhuru wala kutenda lo lote jema.”
6
Hakuna aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ni mkuu, jina lako ni lenye nguvu katika uweza.
7
Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe, Ee mfalme wa mataifa? Hii ni stahili yako. Miongoni mwa watu wote wenye hekima katika mataifa na katika falme zao zote, hakuna aliye kama wewe.
8
Wote hawana akili tena ni wapumbavu, wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lo lote.
9
Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi na dhahabu kutoka Ufazi. Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: vyote vikiwa vimetengenezwa na mafundi stadi.
10
Lakini BWANA ni Mungu wa kweli, yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. Akiwa amekasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
11
“Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia kutoka duniani na kutoka chini ya mbingu.’ ”
12
Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, akaufanya ulimwengu kwa hekima yake na kwa ufahamu wake akazitandaza mbingu.
13
Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua naye huleta upepo kutoka katika ghala zake.
14
Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni madanganyo, wala havina pumzi ndani yake.
15
Havina maana, ni vitu vya mzaha tu, hukumu yao itakapokuja, wataangamia.
16
Yeye aliye Fungu la Yakobo si kama hivi, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
17
Kusanyeni mali na vitu vyenu muondoke katika nchi hii, enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi.
18
Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote waishio katika nchi hii; nitawataabisha ili waweze kutekwa.”
19
Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu! Jeraha langu ni kubwa! Lakini nilisema, “Kweli hii ni adhabu yangu, nami sharti nistahimili.”
20
Hema langu limeangamizwa; kamba zake zote zimekatwa. Wana wangu wametekwa na hawapo tena; hakuna hata mmoja aliyebaki kulisimika hema langu wala wa kusimamisha kibanda changu.
21
Wachungaji hawana akili wala hawamulizi BWANA, hivyo hawastawi na kundi lao lote la kondoo na mbuzi limetawanyika.
22
Sikilizeni! Taarifa inakuja: ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! Hii itafanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.
23
Ninajua, Ee BWANA, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.
24
Unirudi, Ee BWANA, lakini kwa kipimo cha haki: si katika hasira yako, usije ukaniangamiza.
25
Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa yale wasiokujua wewe, juu ya mataifa yale wasioliitia jina lako. Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo; wamemwangamiza kabisa na kuiharibu nchi yake.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52