bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Jeremiah 2
Jeremiah 2
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 3 →
1
Neno la BWANA lilinijia kusema,
2
“Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu.
3
Israeli alikuwa mtakatifu kwa BWANA, malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, nayo maafa yaliwakumba,’ ” asema BWANA.
4
Sikia neno la BWANA, Ee nyumba ya Yakobo, nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.
5
Hivi ndivyo asemavyo BWANA: “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, hata wakatangatanga mbali nami hivyo? Walifuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai.
6
Hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia katika nyika kame, kupitia katika nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’
7
Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu mpate kula matunda yake na utajiri wa mazao yake. Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu na kuufanya urithi wangu chukizo.
8
Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa.
9
“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema BWANA. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.
10
Vuka, nenda ng'ambo mpaka pwani ya Kitimu nawe uangalie, tuma watu waende Kedari na wachunguze kwa makini, uone kama kumekuwapo kitu kama hiki.
11
Je, taifa limebadili miungu yake wakati wo wote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu.
12
Shangaeni katika hili, Ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema BWANA.
13
“Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka visivyoweza kuhifadhi maji.
14
Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa? Kwa nini basi amekuwa mateka?
15
Simba wamenguruma; wamemngurumia. Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketezwa nayo imeachwa haina watu.
16
Pia watu wa Memfisi na Tahpanhesi wamevunja taji ya kichwa chako.
17
Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe kwa kumwacha BWANA, Mungu wako alipowaongoza njiani?
18
Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji kutoka katika Shihori? Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji yatokayo katika Mto Eufrati?
19
Uovu wako utakuadhibu; kurudi nyuma kwako kutakukemea. Basi kumbuka, utambue jinsi lilivyo ovu na chungu kwako unapomwacha BWANA Mungu wako na kutokuwa na hofu yangu,” asema Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote.
20
“Zamani nilivunja nira yako na kukatilia mbali vifungo vyako; ukasema, ‘Sitakutumikia’! Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda matawi yake ulijilaza kama kahaba.
21
Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana, mkamilifu na wa mbegu nzuri. Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami, ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu?
22
Hata ujisafishe kwa magadi na kutumia sabuni nyingi, bado doa la hatia yako liko mbele zangu,” asema BWANA Mwenyezi.
23
“Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi, sijawafuata Mabaali’? Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni; fikiri uliyoyafanya. Wewe ni ngamia jike mwenye mbio ukikimbia hapa na pale,
24
punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo, katika tamaa yake kubwa: akiwa katika wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezae kumzuia? Madume yo yote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake watampata tu.
25
Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu na koo lako liwe limekauka. Lakini ulisema, ‘Haina maana! Ninaipenda miungu ya kigeni, nami ni lazima niifuatie.’
26
“Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa, hivyo ndivyo na nyumba ya Israeli inavyoaibishwa, wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao.
27
Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’ tena wanaliambia jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’ Wamenipa visogo vyao wala hawakunigeuzia nyuso zao; lakini wakiwa katika taabu, wanasema, ‘Njoo utuokoe!’
28
Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa wakati mnapokuwa katika taabu! Kwa maana mna miungu mingi kama mlivyo na miji, Ee Yuda.
29
“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu? Ninyi nyote mmeniasi,” asema BWANA.
30
“Ni bure tu nimeadhibu watu wako, wala hukujirekebisha. Upanga wako umewala manabii wako kama simba mwenye njaa.
31
“Enyi wa kizazi hiki, kumbukeni neno la BWANA: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza kuu? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’?
32
Je, mwanamwali husahau vitu vyake vilivyofanyizwa kwa vito, bibi arusi husahau mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi, tena kwa siku zisizo na hesabu.
33
Je, wewe ni fundi kiasi gani katika kufuatia mapenzi! Hata wale wanawake wabaya kuliko wote wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.
34
Katika nguo zako watu huona damu ya uhai ya maskini wasio na hatia, ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba. Lakini pamoja na haya yote
35
unasema, ‘Sina hatia; Mungu hajanikasirikia.’ Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema, ‘Mimi sijatenda dhambi.’
36
Kwa nini unatangatanga sana, kubadili njia zako? Utakatishwa tamaa na Misri kama ulivyokatishwa na Ashuru.
37
Pia utaondoka mahali hapo ukiwa umeweka mikono kichwani, kwa kuwa BWANA amewakataa wale unaowatumainia; hutasaidika kwa kupitia wao.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52